Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi William Lukuvi ametoa majibu ya mgogoro wa Ardhi wa Shamba la Singu lililopo Mkoani Manyara wilayani Babati kata Ya Sigino
Akiwa Katika ziara yake ya kazi Mkoani humo waziri Lukuvi alitoa uamuzi wa mwisho kuhusiana na mgogoro wa shamba hilo uliodumu kwa muda mrefu kati ya mwekezaji na wananchi .
Alisema Wizara yake ilituma wataalamu wake waliokuja kufuatilia historia ya mgogoro huo na hivyo kugundua kuwa shamba hili lilikuwa linamilikiwa na Luten canal Richard cuper 1926 na baadaye kuuzwa kwa Tanzania Breweries mwaka 1978 Na mwaka 2011 liliuzwa kwa Kampuni ya Agric Evolution Co Ltd ekari 3113.
Aliongeza kuwa kabla shamba hili kuvamiwa na wananchi kulikuwa na jumla ya hekari 3352 na kaya 11, na Sasa kuna jumla ya kaya 410 zilizogengwa katika shamba hilo na kufanya shughuli zao za maendeleo
Kufuatia uvamizi huo Halmashauri ilipanga kubomoa na kuwaondoa wananchi hao waliovamia shamba hilo jambo ambalo Waziri Lukuvi alilipinga na kuwaagiza kuziacha kaya hizo 410 na kuwazuia wananchi wengine watakaoendelea kuvamia.
"Hatuwezi kuwaondoa na kuwabomolea nyumba zao Wananchi wa kipato cha chini, ardhi ambayo ilishajengwa itaondolewa kwenye umiliki wa Muwekezaji""Serikali tumeamua kutoa ekari 829 kwaajili ya wananchi waliojenga katika eneo lile ili waweze kujiendeleza na kufanya shughuli za kilimo na nnaomba mashamba haya muyagawe kwa haki wapewe wahitaji tu, hatuwezi kuwaacha wananchi wetu bila mashamba" alisema Lukuvi.
Waziri lukuvi asema shamba hilo ni mali halali ya Kampuni ya Agric Evolution CO Ltd na hivyo kumtaka muwekezaji huyo kukubaliana na maamuzi ya Serikali kwani Uvamizi huo ulisababishwa na wao kutosimamia mali yao ipasavyo.
Lukuvi amezitaka Halmashauri kufuata sheria na kuwa na desturi ya kumtumia Mwanasheria Mkuu wa Serikali wanapoingia mikataba ya ardhi na wawekezaji ili kuepusha migogoro isiyo na tija na kusababisha Serikali kushtakiwa.
Aidha aliiagiza Tanesco kuwalipa fidia wananchi ambao mashamba yao yamepitiwa na njia za umeme ambapo asilimia 52 ya fedha hizo zitakwenda kwa wananchi na asilimia 48 kwa mwekezaji.
Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti amewataka wanasiasa kuacha kuchochea wananchi kuvamia maeneo ya wawekezaji na yale ya Hifadhi kwa matakwa ya kujisafisha na kujitafutia kura kwa wananchi.
"Hii migogoro mingine ilishaisha lakini kuna baadhi ya wanasiasa ndio wanazidi kuichochea,kwa maslahi yao binafsi, msiwatete wananachi wanapotenda maovu kwa kuwa mnataka kura zao" alisema Mnyeti
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.