Na Fabian Isaya - Mjini Babati
Ni ziara ya Naibu waziri ofisi ya waziri Mkuu vijana ajira na walemavu Mh Patriobasi Katiambi amefanya ziara Mkoa wa Manyara 11/8/2023, akiambatana na Naibu Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu.
Ambapo amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh Queen Sendiga. Ziara hiyo yenye lengo wa ukaguzi wa maandalizi ya shughuli za sherehe za kilele cha mbio za mwenge zinazotarajiwa kufanyika Mkoa wa Manyara mwenzi oktoba 14, 2023.
Sambamba na kupokewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara. Amepokea taarifa fupi kuhusu maandalizi yanayoendelea kufanyika, ikiwa nipamoja na upandaji wa nyasi ambao umekwisha fanyika katika uwanja ambao unaandaliwa kwajili ya kilele cha mbio hizo.
Pia ameeleza juu ya kupatiwa vifaa kutoka kwa wadau nakupewa vijana wa JKT kwajili yakufanya maandalizi yanayoendana na muda uliyowekwa kwajili ya ukamilishaji wa uwanja.
Hata hivyo Mh Queen Sendiga amemueleza Naibu Waziri kuwa kunachangamoto katika ujenzi wa kiwanja hicho cha kwaraa, changamoto kubwa ikiwa ni uhaba wa fedha ameishukuru Serikali kwakutoa Milioni 600 kwajili ya maandalizi ya uwanja huwo.
Pia ameeleza uwekaji wa nyasi umefanyika kwa msaada wa shirikisho la mpira wa miguu TFF. Ameshukuru ofisi ya Waziri Mkuu kwa jinsi ambavyo inashirikiana na ofisi yake ya Mkoa kwa ukaribu ilikuweza kufanikisha shughuli hiyo kubwa kitaifa.
Aidha amemuhakikishia Mh Patriobasi Katambi kuwa maandalizi kwa ujumla yanaenda katika hali ambayo niyenye hatua ya kuridhisha. Katika ziara hiyo Mh Pastriobasi katambi (Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu ajira na walemavu) ametembelea uwanja wa kwaraa ambapo aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Babati Mh Lazaro Twange.
Amefurahishwa na jinsi ujenzi huwo wa uwanja unavyoendelea kwa kasi inayo ridhisha. Amefanya ukaguzi wa majukwaa na hasa ujenzi wa jukwaa kuu pia amepongeza uongozi wa Mkoa kwa namna unavyo weka jitihada zakutosha katika maandalizi hayo. Ametoa rai kwa uongozi wa Mkoa kuwa kilele chambio za mwenge kufanyika katika Mkoa wa Manyara ni niheshima kubwa iliyopewa Mkoa.
Hivyo amehamasisha wananchi wa Mkoa wa Manyara na mikoa ya kaskazini kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kwani ni fursa kwa wafanya biashara na watu mbalimbali wakiwemo vijana.
Amefanya ukaguzi wa uwanja ambao utatumika kwa maonyesho ya wiki ya vijana kitaifa uwanja wa stendi ya zamani, Pia ukaguzi wa eneo la mafunzo kwajili ya vijana wa alaiki ambapo amesisitiza kuwa alaiki kwa vijana haina ushirikiano wowote na masuala ya kichama.
Amezungumza hilo ikiwa nikuwaondowa wazazi katika mtazamo huwo. Bali lengo la alaiki kwa vijana nikupata vijana wazalendo ambao wanaweza kutumika katika ulinzi na usalama kwa badae katika Taifa.
Mkuu wa Wilaya ya Babati Mh Lazaro Twange akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa katika ukaguzi wa maendeleo ya maandalizi hayo ya kilele chambio za mwenge.
Ameaidi kufanyia kazi maelekezo yaliyotolewa na ofisi ya Waziri Mkuu sambamba na hilo amezungumzia kuwepo kwa maandalizi hayo itakuwa na faida kubwa hata mala baada ya kilele chambio za mwenge, akisisitiza hasa katika ujenzi wa uwanja wa kwaraa ambao utaleta manufaa makubwa katika Mkoa.
Ametaja manufaa hayo nipamoja na kukuza Sekta ya michezo katika Mkoa wa Manyara. Ambapo itasaidia kwakiasi kikubwa kuleta ajira kwa vijana wa Mkoa wa Manyara ikizingatiwa kuwa michezo nisehemu pia ya ajira.
Pia itasaidia idadi ya wajasiriamali kuongezeka katika Mkoa wa Manyara kupitia maduka ya biashara yatakayokuwa yakizunguka eneo la uwanja na mapato kuongezeka kwa makusanyo ya kodi ambayo yatatokana na ongezeko la kodi za wananchi.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.