Julai 24. 2023 saa nne asubuhi katika eneo la kijiji cha Bonga nje kidogo ya mji wa Babati Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh Queen Sendiga.
Akiambatana na katibu Tawala Mkoa wa Manyara (Mh Karoline Mthapula) na viongozi wa Ccm Mkoa wa Manyara akiwemo mwenye kiti wa Ccm Mkoa wa Manyara na kamati nzima ya siasa Mkoa wa Manyara amepokelewa Comrade Abrahamani Kinana.
Ziara hiyo ya Comrade Abrahamani Kinana Makamu Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Tanzania bara nikwajili ya kuimarisha chama cha mapinduzi katika Mkoa wa Manyara, Amepokelewa na wananchi wa Bonga kwa furaha huku wananchi wengi wakijitokeza katika eneo hilo.
Mala baada ya mapokezi katika eneo la kijiji cha Bonga Comrade Kinana. Amefanya kikao katika jengo la Ccm Mkoa wa Manyara na wakuu wote wawilaya na wakurugenzi wa Halmashauri zote katika Mkoa wa Manyara katika kikao hicho Comrade kinana amepokea taarifa fupi kutoka kwa katibu wa Ccm Mkoa wa Manyara.
Aidha katibu wa Ccm Mkoa wa Manyara katika kuwasilisha kwake taarifa hiyo fupi ameshukuru chama cha mapinduzi kuendelea kutekeleza irani ya chama kwakuweza kuleta miradi mingi ya maendeleo katika Mkoa wa Manyara.
Pia amemshukuru Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hasani kwakutoa fedha nyingi katika Mkoa wa Manyara katika maeneo mbalimbali ikiwemo elimu Afya ujenzi wa shule katika kila wilaya na vituo vya Afya katika ngazi ya kata na wilaya.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara katika kuwasilisha taarifa ya Serikali, Amemshukuru Mh Rais Samia Suluhu Hasani kwakutoa fedha za utekelezaji wa miradi, Ameleeza kuwa hali ya usalama katika Mkoa wa Manyara ni nzuri na hakuna shida yoyote pia ameshukuru kwa maboresho ya miundo mbinu ya elimu kwa jinsi ilivyofanikiwa katika Mkoa wa Manyara.
Katika kuwashilisha taarifa hivyo Mh Queen Sendiga amemueleza makamu mwenyekiti Tanzania bara Comrade Abrahamani kinana kuwa Mkoa wa Manyara, katika makusanyo yake ya fedha katika ngazi ya Mkoa umefanikiwa kukusanya Bilioni kumi na tisa hiyo nikutokana na ripoti ya mkaguzi Mkuu wa Serikali ya mwaka wa fedha uliyopita ikiwa ni ongezeko zaidi ya makusanyo yaliyopita.
Sambamba na hayo Mh Queen Sendiga amemuelezea Comrade kinana kuwa kunachangamoto pamoja nakuwa na mafaniko hayo katika Mkoa,
Miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na upungufu wa waalimu kwa baadhi ya maeneo katika Mkoa wa Manyara changamoto ya uhaba wa wataalamu wa Afya katika Mkoa wa Manyara changamoto za migogoro ya Aridhi.
Baada ya mazungumzo hayo Mh Queen Sendiga amemkabidhi Comrade Abrahamani kinana ripoti ya Serikali huku tukio hilo likishuhudiwa na wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Manyara.
Pamoja na tukio hilo Comrade kinana amefanya kikao na wanachama cha mapinduzi Mkoa wa Manyara katika ukumbi wa mikutano uliyoko katika jengo la Ccm Mkoa wa Manyara, Amewapongeza wanachama wa Ccm Mkoa wa Manyara kwakuimarisha chama katika ngazi zote wilaya na mpaka kwenye kata na vijiji.
Amewakumbusha majukumu yao wakuu wa wilaya kuwa wao ni nguzo kati ya chama na Serikali ameeleza pia kila zuri ambalo wanachama wa Ccm Mkoa wa Manyara wameliona au kushuhudia limetokana na sera nzuri ya chama cha mapinduzi.
Katika ziara yake Comrade kinana ametembelea eneo la Daleda kati kata ya Ayalagaya ambapo aliambatana na Mkuu wa Mkoa na kamati nzima ya chama cha mapinzudi Mkoa wa Manyara.
Mbunge wa Babati vijijini ambae ndiye mwenyeji wa eneo hilo Mh Daniel Siro amempongeza Mh Rais Samia Suluhu Hasani kwa utekelezaji mzuri wa irani ya chama cha mapinduzi.
Sambamba na hayo Mbuge huyo amewatoa hofu kuhusu tatizo la maji kwa wananchi wa kata ya Ayalagaya kwakuweza kufanikisha mradi mkubwa wa maji ndani ya muda mfupi katika kata hiyo.
Ameeleza juu ya kufanikisha ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Babati vijijini lakini pia upokeaji wa fedha za tasaf kwa kaya zisizo jiweza kiuchumi ufanikishaji wa ujenzi wa madarasa katika kata hiyo.
Aidha Comrade Abrahamani kinana katika kuongea na wananchi wa kata ya Ayalagaya amemshukuru Mbunge Daniel Siro kwa kazi nzuri anayoifanya,
Amezungumzia utekelezaji wa mradi wa maji kupitia mdau aliyejitokeza katika kata ya Ayalagaya. Amemuhakikishia mdau huyo kufanya kazi kwa uhuru na kuongeza miradi mingine katika Sekta ya elimu na Afya amezungumzia juu ya changamoto ya wawekezaji kuingilia maeneo ya wakulima katika kata ya Ayalagaya kuwaachia maeneo ilikuepuka migorogoro kati ya wananchi na wawekezaji.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.