Mheshimiwa Waziri Mkuu katika Ziara yake ametembelea pia Wilaya yaBabati na kupatafursa ya kufikaKiwanda cha Mbolea –Minjingu katika Kijiji cha Minjingu na Kiwanda cha Sukari cha Manyara katika Kijiji cha Matufa na kufanya mikutano ya hadhara katika Vijiji vya Minjingu, Matufa, Madunga, Bashnet, Singu na Arri na kutoa majibu ya kero mbalimbali za Wananchi.
Mheshimiwa Majaliwa alikumbana na Changamoto mbalimbali zilizoelezwa na Wananchi katika maeneo hayo ikiwa ni pamoja na shida ya maji, barabara, upungufu wa watumishi katika sekta ya afya, na malalamiko katika shamba la Singu na Arri ambapo aliitolea ufafanuzi changamoto hizo na kuahidi kuendelea kuzitatua ili kuwaletea wananchi Maendeleo.
Aidha Mheshimiwa Majaliwa alikasirishwa na hali aliyoikuta katika Kiwanda cha Minjingu yakutumia vifungashio vinavyotangaza uzalishaji wa mbolea ya Minjingu – Babati kuwa inazalishwa nchini Kenya badala ya Tanzania na kutoa Maagizo kwa Mkurugenzi wa Kiwanda, kumwandikia Mheshimiwa Rais John Pombe Joseph Magufuli barua ya kuomba radhi pia Mhe. Majaliwa apate nakala ya barua hiyo kabla ya kumaliza Ziara yake, tarehe 22 Februari, 2017.Hata hivyo agizo hilo lilitekelezwa na Mheshimiwa Majaliwa alipata nakala hiyo tarehe 21.2.2017.
Hata hivyo,Mheshimiwa Majaliwa alipowasili katika Kiwanda cha Sukari cha Manyara alifarijika sana kuona Mkoa una Kiwanda hicho ikiwa ni juhudi za kuunga Mkono dhamira ya Mheshimiwa Rais ya kuifanya Nchi yetu kuwa ya viwanda na kupunguza uhaba wa Sukari na kutoa ajira kwa wazawa ili waweze kujikwamua na umaskini.
Mheshimiwa Majaliwa,alihitimisha ziara yake katika Mji wa Babati kwa kuweka jiwe la msingi Mradi wa Daraja(boksi Kalvati mbili) katika barabara ya Bonga – Endanachan.Pamoja na Majumuisho na Watumishi alisisitiza uadilifu kwa watumishi katika kuwatumikia wananchi na mapambano dhidi ya dawa za kulevya.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.