Kuelekea Kilele cha Mbioa za Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga amefanya ziara ya ukaguzi wa vituo vya Afya katika Halmashaui ya Babati vijijini. Ambapo ametembelea Zahanati ya Gidemara amefanya ukaguzi wa ujenzi wa sehemu ya kunawiya mikono na ujenzi wa vyoo vitatu, chumba cha kujifungulia wakina Mama na tenki la kuhifadhia maji, Zahanati ya Gidemara iko katika kata ya Galapo, mradi ulianza Juni 2022 na unategemea kumalizika Sepetmba 2023.
Amewataka kamati ya ujenzi kumaliza mradi huo kwa wakati ili wananchi wa kata ya Galapo waweze kupata huduma za Afya na waondokane na usumbufu walinao upata. Amefurahishwa na maendeleo ya ujenzi wa Zahanati hiyo kwa jinsi unavyoendelea.
Aidha Mkuu wa Mkoa ametembelea Zahanati ya Nkasi iliyopo katika kata ya Mamile amefanya ukaguzi wa ujenzi wa sehemu ya kuchomea taka, chumba cha kujifungulia kwaajili ya wazazi, tenki la kuvunia maji ya mvua, Pia amefurahishwa na ujenzi wa Zahanai hiyo kwa jinsi unavyoendelea na ukiwa kwenye hatua zakumalizika ili wananchi wa Mamile waanze kupata huduma.
Pia ametembelea Zahanati ya Mamile iliyopo kata ya Mamile amefanya ukaguzi wa kichomea taka na temki la kuvunia maji, Zahanati ya Mamile ni miongoni mwa vituo vya Afya vinavyotoa huduma katika Wilaya ya Babati, Aidha katika kuwasirishiwa taarifa ameeleza juu ya uwepo wa upungufu wa nyumba za watumihi , upungufu wa watumishi katika Zahanati hiyo.
Sambamba na ukaguzi amefanya mkutano na wananchi wa kijiji cha Mwinkantsi katika mkutano na wananchi nakupata wasaa wakusikiliza kero za wananchi wa kijiji cha Mwinkantsi. Ambapo miongoni mwa changamoto alizopokea ni changamoto za upatikanaji wa huduma ya maji na huduma ya umeme katika kijiji hicho.
Katika mkutano huo amewataka watendaji kuhudumia wananchi na kusikiliza kero za wananchi, Ametoa maelekezo kwa mamlaka husika kutatua changamoto ya maji na umeme katika kijiji cha Mwinkantsi. Pia amewataka wazazi kuongea na vijana wao ilikuondoa tatizo la ukatili wa kijnsia ambalo linaonekana kuwa kubwa katika Mkoa wa Manyara.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.