Waziri Mkuu wa Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) amefanya ziara yakeHalmashauri ya Wilaya ya Mbulu na kupata fursa ya kutembelea Hospitali Teule ya Wilaya inayomilikiwa na K.K.K.T iliyopo Haydom, kuongea na Watendaji wa Halmashauri za Wilaya za Mbulu na Mbulu Mji, kuongea na wananchi katika mikutano ya hadhara katika vijiji vya Haydom na Dongobeshi; na mkutano mmoja katika viwanja vya Halmashauri ya Mji wa Mbulu.
Mheshimiwa Majaliwa alipokea Taarifa ya Hospital yenye ombi la kutaka Hospitali hiyo kupandishwa Hadhi na kuwa Hospital ya Kanda kwa kuwa inahudumia Mikoa ya Tabora, Arusha, Manyara, Singida na Simiyu; na uwepo wa chuo cha uuguzi, madaktari na utafiti.
Hata hivyo, Mheshimiwa majaliwakuhusiana na ombi hilo alimwagiza Waziri wa Afya kufanya tathmini kubaini kama hospitali inakidhi vigezo, na kuahidikushughulikia changamoto nyinginezo zikiwemo, ruzuku ya madawa ili wananchi wazidi kupata huduma staiki.
Kwa upande mwingine,Mheshimiwa Majaliwa alitembelea Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara iliyofanyika katika vijiji vya Endagaw na Katesh Mjini. alikagua Soko la Kimataifa jipya, kuzindua mradi wa ujenzi wa madarasa nane (8), ukarabati wa madarasa matatu (3), Ofisi ya moja (1) na ujenzi wa matundu 14 ya vyoo katika Shule ya Msingi Mogitu.
Hata hivyo alifarijika sana na Utekelezaji wa mradi wa shule ya msingi Mogitu na kueleza kuwa ni kielelezo cha usimamizi bora wa miradi na fedha za umma na umeonesha thamani ya pesa (value for money) kwa sababu umetekelezwa kwa muda mfupi na kuleta matokeo ya mfano katika Wilaya na Mkoa kwa ujumla.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.