Saturday 23rd, November 2024
@Gallapo
Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza kuwa shughuli za maadhimisho ya sherehe za miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yafanyike katika ngazi ya mikoa kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi. Maadhimisho hayo ambayo yameanza kufanyika kuanzia tarehe 17 Aprili, 2023 hadi siku ya kilele tarehe 26 Aprili, 2023, yatafanyika kupitia Mikoa, Taasisi za Serikali na Vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama yataambatana na uzinduzi wa miradi ya maendeleo, shughuli za kijamii hususan upandaji miti, usafi wa mazingira na mashindano ya michezo na sanaa mbalimbali.
Kadhalika, yataambatana na Mashindano ya uandishi wa Insha kwa shule za Msingi na Sekondari, mahojiano maalum na Wazee maarufu, midahalo na makongamano kuhusu Muungano na hatua ya maendeleo iliyofikiwa hadi sasa. “Majengo yote ya Serikali yapambwe kwa vitambaa vyenye rangi sahihi za bendera ya Taifa, picha za Waasisi wa Muungano, Picha ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande wa Tanzania Bara” Alisema Waziri Mkuu.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.