Dira
“Kuwa Taasisi ya Mfano nchini kwa kutoa huduma bora katika kushauri masuala ya kiuchumi na kijamii kwa wadau wake wote”.
Dhima
“Kuimarisha mifumo ya Serikali za mitaa na kuratibu huduma maendeleo ya Jamii na za kiuchumi kwa wadau wetu kwa kutoa ushauri, huduma za kitaalam na kuelekeza mambo ya kisheria kwa wananchi wote wa mkoa wa Manyara”.
Majukumu ya Sekretarieti ya mkoa
Kutafsiri sera,kuzijengea uwezo na kuzisaidia serikali za mitaa kutekeleza majukumu yake ya kijamii na kiuchumi na huduma za maendeleo na kuhakikisha kuwa kuna amani a utulivu katika mkoa.
Wajibu na Kazi
Wajibu na kazi za sekreatarieti ya mkoa ni mengi na yamekasmiwa kwa kila Klasta na Kitengo(section and Unit) .Kwa ujumla jukumu kubwa linalenga kumsaidia mkuu wa mkoa kama ifuatavyo:-
1.Kutekeleza kazi za serikali ndani ya mkoa.
2.Kusimamia utawala wa sheria mkoani
3.Kutoa mwelekeo wa jitihada katika kutekeleza sera mbalimbali mkoani.
4.Kuzishauri a kuzisaidia Serikali za mitaa kutekeleza mipango yake kwa lengo la kuleta maendeleo na kuodoa umaskini.
5.Kutekeleza kazi namajukumu mengine ya RS ya kisheria.
Majukumu ya kimaendeleo yanajumuisha usimamizi na tathmini,uwezo wa kiutawala wa kutekeleza kutoa huduma.Tathmini ya utoaji huduma inajikita kwenye kufikiwa kwa malengo na matokeo ya malengo hayo katika jamii.
Majukumu ya kiutawala yana sehemu kuu tatu:-
1. Kulinda amani na utulivu katika mkoa ili wananchi watekeleze majukumu yao.
2. Kuziwezesha na Kuzisaidia Serikali za mitaa katika mkoa kutekeleza majukumu yake kwa kuzijengea mazigira bora ya kutekeleza majukumu na wajibu wake.
3. Kuiwakilisha serikali kuu katika mkoa.
Majukumu ya kisera ya Mkoa ni pamoja na:
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.