Kitengo hiki kina lengo la kutoa huduma ya ushauri kwa Afisa Masuuli kuhusu taratibu sahihi na zinazokubalika za usimamizi wa masuala ya fedha. Kitengo hiki kinaongozwa na Mkaguzi Mkuu wa Ndani Sekretarieti ya Mkoa ambaye anawajibika kwa Katibu Tawala wa Mkoa.
Majukumu ya Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
Kupitia na kutoa taarifa juu ya udhibiti sahihi wa mapokezi, utunzaji na matumizi ya rasilimalifedha za Sekretarieti ya Mkoa
Kupitia na kutoa taarifa juu ya na kiutendaji na kuandaa taarifa za fedha na nyinginezo.
Kupitia na kutoa taarifa juu ya mifumo iliyopo inayotumika kutunza rasilimali na kujiridhisha uwepo wa rasilimali hizo husika
Kupitia na kutoa taarifa juu ya majibu ya menejimenti kwenye taarifa za ukaguzi wa ndani na kuisaidia menejimenti kwenye utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa kwenye taarifa mbalimbali na ufutiliaji kwenye utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Kupitia na kutoa taarifa juu ya uwezo/ufanisi wa udhibiti uliopo kwenye mifumo iliyounganishwa na kompyuta kwenye Sekretarieti ya Mkoa.
Kuandaa na kutekeleza Mipango Mkakati wa Ukaguzi wa Ndani