Wakazi wa Mkoa wa manyara pia wanajishughulisha na ufugaji wa ngombe wa asili na kisasa ambao hutoa mazao ya nyama na maziwa, wananchi pia hufuga mbuzi, kondoo, punda, nguruwe pamoja na kuku kwa ajili ya kujipatia kipato. Aidha, katika Mkoa wetu kuna jumla ya ng’ombe 1,925,345, mbuzi 1,472,490, Kondoo 651,863 na punda 64,054 ambapo shughuli kubwa ya ufugaji inafanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro na Kiteto kutokana na uwepo wa jamii ya kimasai.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.