Kuna vivutio vya aina mbalimbali vya utalii vinavyopatikana katika Mkoa wa Manyara kama vile Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, Hifadhi ya Manyara, maeneo ya Jumuiya za Hifadhi za wanyapori (Burunge na makame), maeneo ya uwindaji wa kitalii ambayo yapo Simanjiro (9), Kiteto (4) na Babati (1), utalii wa kitamaduni kwa makabila yaliyopo ndani ya mkoa yanayodumisha mila zao ambao ni Masai, Hadzabe, Barbaiq, Ndorobo, utalii wa kupanda milima Hanang’. Vivutio vingine vya utalii ni pamoja na mlima Kwaraa na Safu za mlima Nou. Wananchi hunufaika kupitia shughuli za kuongoza watalii, kutoa huduma za malazi, uuzaji wa bidhaa za kilimo, shanga, uchongaji wa vinyago
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.