Bw.ALLY SALEHE MOKIWA
Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji
Seksheni ya Uchumi na Uzalishaji
Seksheni ya Uchumi na Uzalishaji ina lengo la kutoa uwezeshaji wa kitaalamu kuhusu sekta za uchumi na uzalishaji kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Mkoa. Seksheni hii inaongozwa na Katibu Tawala Msaidizi ambaye anawajibika kwa Katibu Tawala wa Mkoa
Majukumu ya Seksheni ya Uchumi na Uzalishaji
•Kuratibu utekelezaji wa sera za Kilimo, Mifugo, Ushirika, Misitu, Uhifadhi, Uvuvi, Viwanda, Biashara na Masoko katika Mkoa
•Kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Mkoa katika kutoa huduma kwenye nyanja za Kilimo, Mifugo, Ushirika, Misitu, Uhifadhi, Uvuvi, Viwanda, Biashara na Masoko
•Kuzisaidia na kuzishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa juu ya teknolojia zinazofaa na za gharama nafuu katika sekta za uchumi na uzalishaji
•Kusajili vyama/vikundi vya ushirika katika Mkoa
•Kuzishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa katika juu ya uanzishaji/uimarishaji na ukaguzi wa vyama vya Ushirika na Akiba na Mikopo
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.