Zaidi ya asilimia 83 wananchi wa Mkoa wa Manyara hujishughulisha na kilimo cha mazao mbalimbali yakiwemo mazao ya chakula mfano, mahindi, mpunga, maharage, mazao ya mizizi (viazi, mihogo n,k) na mazao ya biashara kama vile, mbaazi, alizeti, kahawa, dengu, ngano n.k.
Mkoa una fursa ya kuwa na maeneo yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji takribani hekta 30,997 ambazo kati ya hizo hekta 11, 715 zinamwagiliwa na hekta 19,282 zinahitaji kuendelezwa kwa kujengewa mindombinu ya umwagiliaji. Aidha, skimu za umwagiliaji zinazofanya kaazi kwa sasa ni pamoja na Ngage, Lemkuna na Kambi ya chokaa (Simanjiro), Shauri Moyo, Mkombozi na Muungano (Babati). Uwepo wa skimu hizo unawasaidia wananchi kuzalisha mazao kwa kipindi chote cha mwaka, kuzalisha kwa tija, hivyo kuwa na uhakika wa chakula na kipato
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.