Wilaya ya Hanang Ni mojawapo ya Wilaya tano zinazounda Mkoa wa Manyara. Hianzishwa rasmi mwaka 1985 Kwa Tangazo la Serikali Na. 33 la tarehe 28/5/1985. Mwaka mmoja baadaye, Halmashauri ya Wilaya ya Hanang ilianzishwa Kwa Tangazo la Serikali la 412 tarehe 15/8/1986. Hanang inapakana Na Wilaya za Mbulu na Babati kwa upande wa kaskazini.
Kondoa na Singida kwa upande wa Kusini, Iramba kwa upande wa Magharibi na Kondoa kwa uapnde wa Mashariki.
Wilaya ya Hanang iko kati ya longotudo 34°.45" Na 35°. 48" Mashariki ya Greenwich na Latitudo 4°.25" na 5° Kusini mwa Ikweta. Wilaya iko katika mwinuko wa kati ya Mita 1000 na 2000 juu
ya usawa wa bahari. Wilaya hupata wastani wa mvua za kati ya milimita 500 -900 ambazo hunyesha kati ya mwezi Novemba na Mei ambapo ukanda wa juu wa mlima Hanang unapata mvua nyingi zaidi. Wilaya ina ukubwa wa kilometa za mraba 3,639 ambazo ni sawa na hekta 363,900.
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, Wilaya ina jumla ya watu 275,990, kati yao wanaume ni 140212 na Wanawake 135,778. Kwa makadirio kwa kipindi cha mwaka 2016, Wilaya inakadiriwa kuwa na jumla ya watu 310,629, Me. 157 157,810 na ke 152,819 ongezeko la watu kwa mwaka ni wastani wa 3.0%. Maaaaaakabila wakaazi wenyeji wa Wilaya ni Wairaq, Wabarbaig, Wanyaturu na Wanyiramba.
Wilaya imegawanyika katika Tarafa tano (5), Kata thelathini na tatu (33), Vijiji tisini na sita (96), Vitongoji 414 na Jimbo moja la Uchaguzi. Makao Makuu ya Wilaya ni Katesh.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.