JIOGRAFIA YA WILAYA:-
Wilaya ya Babati iko Kaskazini mwa Tanzania katika Mkoa wa Manyara kati ya Latitudo 30 – 50 Kusini mwa Ikweta na Longitudo 350 – 370 mashariki ya Greenwish.
ENEO LA WILAYA:
Wilaya ya Babati ilianzishwa kwa kuigawanya iliyokuwa Wilaya ya Hanang katika wilaya mbili - Babati na Hanang. Uamuzi huo ulitoa Wilaya ya Babati, ambayo iliandikwa rasmi katika Gazeti Rasmi la Serikali namba 403 tarehe 1 Oktoba 1985. Wilaya ya Babati ina ukubwa wa kilomita za mraba 6,069. Ni moja kati ya Wilaya tano (5) zinazounda Mkoa wa Manyara. Kwa upande wa Kaskazini Wilaya hii inapakana na Wilaya ya Monduli, Wilaya ya Mbulu kwa upande wa Magharibi, Wilaya ya Hanang kwa upande wa Kusini Magharibi, Wilaya ya Kondoa kwa upande wa Kusini na Wilaya ya Simanjiro kwa upande wa Kusini Mashariki.
UTAWALA:
Wilaya imeundwa na Halmashauri mbili ambazo ni Halmashauri ya Wilaya ya Babati na Halmashauri ya Mji wa Babati. Halmashauri ya Wilaya ina Vitongoji 408, Vijiji 102 na Kata 25. Halmashauri ya Mji ina Vitongoji 54, Vijiji 13, Mitaa 35 na Kata 8. Aidha, Wilaya ina Tarafa nne (4) ambazo ni Babati, Bashnet, Mbugwe na Gorowa na Majimbo mawili ya Uchaguzi wa Ubunge ambayo ni Jimbo la Babati Mjini na Jimbo la Babati Vijijini.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.