Na, Ruth Kyelula, Manyara RS
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Queen Sendiga, ametoa wito kwa waandishi wa habari, kutoka kwenda kuhimiza wananchi kuhusiana na kudumisha Amani wakati wa uchaguzi, kabla na baada ya uchauzi.

Aliyasema hayo mapema leo, ofisini kwake Oktoba 21,2025 wakati akizungumza na waandishi wa Habari, kuhusiana na uchauzi mkuu wa mwaka huu.
“Tumebakiza siku chache, leo ni tarehe 21, tunategemea kufanya uchaguzi tarehe 29, kwahiyo tunakama siku nane tu hapa kuelekea kwenye siku hiyo ya uchaguzi, naomba niwashukuru sana waandishi wa habari kwa kazi kubwa mnayoendelea kufanya kwa kuhabarisha umma, lakini pia kuwakumbusha wanamanyara kwamba tunakwenda kwenye zoezi la uchaguzi, lakini kama serikali tumeona tuna wajibu wa kuzungumza katika siku hizi zilizosalia ambazo ni taribani siku nane .” Alisema Mhe. Sendiga.

Aidha alisema ushiriki wa wananchi wote kwenye uchaguzi huu ni wa muhimu, muendelee kuhamasisha wananchi wajitokeze kupiga kura, ni suala la muhimu sana kama mlivyofanya kwenye kuhamasisha wananchi kuboresha dafftari la kupiga kura.Na sasa muwahamasishe kama walivyojitokeza kwenye kuboresha taarifa zao kwenye daftari, sasa wakapige kura.Na vituo vitakuwa wazi kuanzia saa moja asubuhi na kufungwa saa kumi jioni.

Sambamba na hilo amekemea makundi ama mtu yeyote, ambao wanadhani watatumia tarehe 29, katika kutekeleza adhma zao ovu, kama Mkoa wamejipanga kuhakikisha kwamba yeyote atakaekuwa amejipanga eidha kwa makusudi ama kwa bahati mbaya, kwenda kufanya vurugu ndani ya Mkoa wa Manyara, hawatamvumilia wala kumuacha salama.

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.