Ndugu Msomaji karibu katika Tovuti rasmi ya Mkoa wa Manyara.Sekretarieti za Mikoa zilianzishwa kwa mujibu wa sheria namba 8(1) cha sheria ya Tawala za Mikoa sura ya 97 sheria ya mwaka 1997. Sekretarieti za Mikoa zimepewa majukumu mbalimbali ya kutekeleza ikiwa ni pamoja na kuratibu utekelezaji wa shughuli za wizara za kisekta,kusimamia utekelezaji wa sera za Kitaifa ndani ya eneo la Mkoa,kufuatilia na kutathimini utoaji na upatikanaji wa huduma katika mikoa, kupitia bajeti za Halmashauri na kutoa ushauri kuhusu sera za Taifa,kufuatilia na kutathimini matumizi ya ruzuku ya Serikali za Mitaa zilizo katika Mikoa.Aidha kwa mujibu wa sheria Na 19 ya 1997 Majukumu ya Sekretarieti ya Mkoa ni kumsaidia Mkuu wa Mkoa kutekeleza majukumu yake, majukumu hayo ni kama vile Ulinzi na usalama, uchumi, utamaduni, maendeleo ya Mkoa, pamoja na kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa shughuli zote zinazotekelezwa katika Serikali za Mitaa pamoja na kutoa mwongozo kwa Sekta binafsi.
Mkoa wa Manyara ulianzishwa kwa tangazo la Serikali Na. 367 lililotolewa tarehe 27 Julai, 2002 na kuchapishwa katika gazeti la Serikali tarehe 2 Agosti, 2002 baada ya kugawanywa kwa Mkoa wa Arusha ambao kabla na wakati wa kipindi cha Uhuru ulijulikana kama Jimbo la Kaskazini (Northern Province). Mkoa wa Arusha ulianza kutumia rasmi jina hilo mwaka 1963.Miongoni mwa Wilaya zilizounda Mkoa huo ni Mbulu na Maasailand ambazo sehemu kubwa iko katika Mkoa wa Manyara sasa. Wilaya hizo ziligawanywa kama ifuatavyo:- Wilaya ya Mbulu ilianzisha Wilaya ya Hanang mwaka 1969 na Hanang ikianzisha Babati mwaka 1985, wakati Wilaya ya Maasailand iligawanywa kwenye Wilaya ya Kiteto mwaka 1974 ambayo pia iligawanywa na kuanzisha Wilaya ya Simanjiro mwaka 1993. Aidha, baada ya kugawanywa kwa Mkoa wa Arusha, Wilaya za Mbulu, Hanang’, Babati, Kiteto na Simanjiro ziliuunda Mkoa wa Manyara.
|
|
Mkoa wa Manyara ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 27000.Mkoa wa Manyara unapakana na Mikoa ya Singida na Shinyanga upande wa magharibi, Mkoa wa Dodoma upande wa kusini, Mkoa wa Tanga upande wa mashariki na Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro Upande wa kaskazini.
Makao makuu ya mkoa wa Manyara yapo Babati Mjini.
Idadi ya watu, Mkoa wa Manyara una jumla ya wakazi 1,425,131 kati ya hao Wanaume ni 717,085 na Wanawake ni 708,046 (sensa ya mwaka 2002) Idadi hiyo imepatikana katika wilaya zifuatazo (idadi ya wakazi katika mabano mwaka 2002): Babati (303,013), Hanang (205,133), Mbulu (237,882), Simanjiro (141,676) na Kiteto (152,757).
Sensa zinaonyesha kwamba ni kati ya mikoa ya Tanzania yenye ongezeko kubwa la wakazi. Pia ni kati ya mikoa yenye maambukizi machache zaidi ya Ukimwi.
Makabila Makuu katika Mkoa
WAKAZI WA WILAYA |
KUNDI KUU
|
KUNDI DOGO
|
BABATI
|
Wabantu
|
Wambungwe,Warangi,Wachagga, Wapare, Wangoni,Waasi na Makabila mengine
|
Nilo Hamites
|
Wagorowa, Wa-Iraqw, Maasai, Barbaig
|
|
HANANG’
|
Wabantu
|
Wanyiramba, Warangi, Wanyaturu na makabila mengine
|
Nilo Hamites
|
Wabarbaig, Wa-Iraqw.
|
|
MBULU
|
Nilo Hamites
|
Wa-Iragw, Wabarbaig, Wahadzabe.
|
KITETO
|
Wabantu
|
Wagogo, Warangi, Wanguu, Wakaguru, Wasambaa na makabila mengine
|
Nilo Hamites
|
Wamaasai, Waburunge, Wa-Akea (Wandorobo)
|
|
SIMANJIRO
|
Wabantu
|
Wanguu, Wachagga, Wapare, Warangi na makabila mengine.
|
Nilo Hamites
|
Wamaasai na Wandorobo[ Wa-Akea ]
|
NB: Kwa sasa kuna makabila mengine madogo madogo. Aidha makabila ya Hadzabe na Akea yanahitaji uangalizi kwa vile huishi kwa kutegemea uwindaji, mizizi, matunda na kula asali.
HALI YA HEWA YA MKOA
Mkoa unapata wastani wa Mvua kati ya mm 450 na mm1200 kwa mwaka. Kuna misimu miwili ya mvua. Mvua za muda mfupi ambazo hunyesha kati ya Oktoba na Desemba katika baadhi ya maeneo ya Wilaya za Kiteto, Hanang’, Babati na Mbulu. Mvua za muda mrefu hunyesha kati ya mwezi Februari na Juni. Hali ya hewa ni nyuzi joto 130C wakati wa masika na nyuzi 330C wakati wa kiangazi kutegemeana na msimu na mwinuko wa ardhi. Mkoa upo katika mwinuko kati ya mita 1000 – 2000 juu ya usawa wa bahari
WABUNGE WA WA MKOA WA MANYARA.
Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2020 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi 7 yafuatayo:
Wakuu wa Mkoa walioongoza Mkoa wa Manyara toka 2002 hadi sasa.
Na
|
Jina Kamili |
Mwaka alionza
|
Mwaka alioondoka
|
1.
|
Mhe.Kanali (mst) ANATOLI A. TARIMO
|
22/08/2002
|
10/05/2007
|
2.
|
Mhe. HENRY D. SHEKIFU
|
10/05/2007
|
19/08/2010
|
3.
|
Mhe.ELASTON J. MBWILO
|
19/09/2011
|
06/12/2014
|
4.
|
Mhe.Dkt. JOEL N. BENDERA
|
06/12/2014
|
26/10/2017
|
5.
6. 7 |
Mhe.ALEXANDER P. MNYETI
Mhe.JOSEPH JOSEPH MKIRIKITI Mhe.Charles Makongoro Nyerere |
26/10/2017
16/07/2020 15/05/2021 |
15/07/2020
15/05/2021 Hadi sasa |
Makatibu Tawala Walioongoza Mkoa wa Manyara toka 2002 hadi sasa
Na.
|
Jina Kamili |
Mwaka alioanza
|
Mwaka alioondoka
|
|||||
1.
|
PHINIAS L. NNKO
|
22/08/2002
|
04/12/2007
|
|||||
2.
|
THOMAS G. SOWANI
|
24/09/2008
|
07/07/2010
|
|||||
3.
|
BITEGEKO B. CLAUDIO
|
08/07/2010
|
15/04/2013
|
|||||
4.
|
Mhandisi. OMAR A. CHAMBO
|
03/02/2014
|
23/10/2015
|
|||||
5.
6. 7. |
ELIAKIM C. MASWI
MISSAILE R. MUSA KALORINA A. MTHAPULA |
23/10/2015
28/07/2018 29/05/2021 |
27/07/2018
29/05/2021 Mpaka Sasa
|
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.