• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

HAKIKISHENI VITUO VYA AFYA VYOTE VINAKUWA NA HATI MILIKI-Dkt.Chaula

Imechapishwa Tarehe: October 5th, 2018

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa   na Serikali za Mitaa Dkt. Zainabu Chaula amewaagiza viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha vituo  vyote vya afya  vinapatiwa hati miliki.

Dkt. Chaula ameyasema hayo alipokuwa akikagua ukarabati na ujenzi wa kituo cha afya cha Mabamba kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Mkoani Kigoma katika ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa vituo vya afya nchini leo Mkoani Kigoma.

Amesema kuwa Serikali imetumia gharama kubwa katika ujenzi wa miundombinu ya afya nchini, hivyo Mamlaka za Serikali za Mitaa hazinabudi kuhakikisha zahanati na vituo vyote vya afya nchini vinakuwa na hati miliki.

“Viongozi wamekuwa wakitoa maagizo kuhusu uwepo wa hati miliki kwa majengo ya Serikali lakini bado baadhi ya watendaji wa Mamlaka husika hawatekelezi maagizo hayo, hivyo nawaagiza viongozi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha kila Zahanati, Kituo cha afya kinakuwa na Hati Miliki.” Anasisitiza Dkt. Chaula

Akiongelea kuhusu ukusanyaji wa mapato Dkt. Chaula amesema kuwa kila kituo cha afya kinatakiwa kufunga mifumo ya kielektroniki ili kuongeza mapato kwenye vituo vya afya.

“Sijaridhishwa na hali ya ukusanyaji wa mapato katika Zahanati na vituo vya afya kwa kuwa mapato bado nimadogo ukilinganisha na huduma zinazotolewa ukizingatia kuwa Serikali imeweza kukarabati na kujenga miundombinu ya afya nchini, hivyo nawaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa mapato katika vituo hivyo” Anasema Dkt. Chaula

Naye Mganga Mfawidhi wa Wilaya ya Kibondo Dkt.Sebastian Pima amesema kuwa ujenzi na ukarabati wa awamu ya kwanza umetekelezwa  katika kituo cha Afya cha Mabamba na kugharimu  shilingi milioni 500.

Dkt. Pima ameyataja majengo yaliyojengwa kuwa ni wodi ya kinamama yenye uwezo wa kuchukua vitanda vine (4), Kliniki ya baba, mama na mtoto, nyumba ya mtumishi, chumba cha kuifadhia maiti, chumba cha upasuaji, chumba cha kufulia, maabara na ukarabati wa jengo lazamani la wodi ya wazazi.  

Aidha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Zainabu Chaula yupo kwenye ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa vituo vya afya nchini na tayari ameshatembelea Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko na Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma.

Chanzo:www.tamisemi.go.tz

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.