Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Bwana Musa Missaile ameziagiza Halmashauri zote za Mkoa huo kuhakikisha wanajenga madarasa pamoja na kutengeneza madawati ili wanafunzi wote 557 waliokosa nafasi za kujiunga kidato cha kwanza 2021 katika shule za sekondari zilizopo mkoani Manyara wawe wamesharipoti shule ifikapo mwezi Februari 2021.
Katibu Tawala ameyasema hayo leo alipokuwa katika kikao cha uchaguzi wa wanafunzi wanaotakiwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2021 kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
“Halmashauri hizi ambazo watoto wamekosa nafasi zihakikishe madara na na madawati yake yamekamilika ili watoto waingie madarasani !!” Alisema Katibu Tawala.
Akielezea mbele ya wajumbe waliohudhuria kikao hicho Kaimu Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Elimu Bwana Lago Sillo alisema kuwa kati ya watahiniwa 31981(Wavulana 15,143 na Wasichana 16,838) walioanza darasa la kwanza mwaka 2014, watahiniwa 30800 (Wavulana 14426 na wasichana 16,374) walifanya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi na watahiniwa 1181 (Wavulana 717 na wasichana 464) hawakufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utoro,vifo, ugonjwa n.k
Vilevile Bwana Sillo amesema kuwa watahiniwa wamefaulu Zaidi katika Somo la Kiswahili na Somo la Kiingereza ndo somo lililokuwa la mwisho.
Bwana Lago Sillo pia aliwataja wanafunzi kumi bora wasichana na wavulana waliofanya vizuri ikiwa na Pamoja na shule na Halmashauri walizotoka.
Wanafunzi kumi bora Wasichana katika Mkoa wa Manyara
Na
|
Jina la Mwanafunzi
|
Shule anayotoka
|
Halmashauri
|
1
|
Glory Samweli Mathiya
|
Deira
|
Babati Mji
|
2
|
Laura Leonce Gwandu
|
Deira
|
Babati Mji
|
3
|
Joyce Jackson Fissoo
|
Mount Hanang
|
Hanang
|
4
|
Lilian Deogratias Lyakinana
|
Deira
|
Babati Mji
|
5
|
Doreen Agustino Darema
|
Laalakir
|
Kiteto
|
6
|
Joyce Paschali Sulumo
|
Laalakir
|
Kiteto
|
7
|
Monica Emanuel Muhandi
|
Amka Afrika
|
Babati Mji
|
8
|
Ester Albert Ngara
|
St.Clare
|
Babati Mji
|
9
|
Judith John Butta
|
Deira
|
Babati Mji
|
10
|
Monica Kimirei Masiaya
|
Laalakir
|
Kiteto
|
Wanafunzi kumi bora Wavulana katika Mkoa wa Manyara
Na
|
Jina la Mwanafunzi
|
Shule anayotoka
|
Halmashauri
|
1
|
Deusdedith Korduni Lengaram
|
Blue Tanzanite
|
Simanjiro
|
2
|
Elihuruma Samson Thomas
|
Mount Hanang
|
Hanang
|
3
|
Ibrahim Moses Mollel
|
New Light
|
Simanjiro
|
4
|
Celvin Leonard Sulley
|
Mount Hanang
|
Hanang
|
5
|
Jovin Emanuel Kirenga
|
Blue Tanzanite
|
Simanjiro
|
6
|
Mudathir Izadin Ramadhani
|
Blue Tanzanite
|
Simanjiro
|
7
|
Bosco Thomas Mollel
|
Deira
|
Babati Mji
|
8
|
Elia Cosmas Kessy
|
Amka Afrika
|
Babati Mji
|
9
|
Beatus Sekey Ayo
|
Laalakir
|
Kiteto
|
10
|
Eliseus Amnaay Sarwat
|
Laalakir
|
Kiteto
|
Shule kumi zilizofanya vizuri Kimkoa
Na
|
Shule
|
Halmashauri
|
1
|
Laalakir
|
Kiteto
|
2
|
Kazamoyo
|
Simanjiro
|
3
|
Deira
|
Babati Mji
|
4
|
New Vision
|
Simanjiro
|
5
|
Barazani
|
Mbulu Wilaya
|
6
|
Kweli L. Centre
|
Hanang
|
7
|
St.Clare
|
Babati Mji
|
8
|
Aldersgate
|
Babati Mji
|
9
|
Mount Hanang
|
Hanang
|
10
|
New Light
|
Simanjiro
|
Akielezea jinsi Halmashauri zilivyofaulisha katika Mkoa wa Manyara Bwana Lago Sillo alisema kuwa Halmashauri ya Mji wa Babati imeshika nafasi ya kwanza kwa kupata asilimia 84.33 ikifuatiwa na Halmashauri ya Mji wa Mbulu iliyopata asilimia 81.47 na ya tatu ni Halmshauri ya wilaya ya Babati iliyopata asilimia 74.5 huku Halmashauri ya Wilaya ya Hanang ikiwa ya mwisho kwa kupata asilimia 67.43 ikifuatiwa na Halmashuari ya Wilaya ya Mbulu asilimia 68.92 na Kiteto asilimia 71.74.
Angalia majina ya Kila Mwanafunzi na shule aliyochaguliwa kwenye sehemu ya Matangazo
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.