WAKUU wa Mikoa kote nchini wametakiwa kutumia fursa ya tamko la Serikali la kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki kwa kuhamasisha ujenzi wa viwanda vya mifuko rafiki wa mazingira.
Pia wametakiwa kushiriki kikamilifu katika kutekeleza agenda ya serikali ya kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki katika maeneo yao.
Wito huo umetolewa jana jijini hapa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo na kusema ni vyema wakuu wa mikoa wakamasisha ujenzi wa viwanda vya mifuko mbadala ambavyo vitasaidia upatikanaji wa bidhaa hiyo na kutoa ajira katika maeneo yao
“Sasa mifuko ya plastiki haitatumika tena, pia kuna fursa ya ujenzi wa viwanda, jambo hili litupe nafasi sisi wakuu wa mikoa kama mifuko ya plastiki haitumiki tuangalie jinsi gani katika kampeni yetu ya ujenzi wa viwanda vidogo, kati na vikubwa tukatumia fursa hii.
Aliongeza: “Mnakumbuka katika kampeni yetu ya miezi 12 ya kila mkoa kujenga viwanda vidogo, vya kati na vikubwa vipatavyo 100, lengu letu ilikuwa vijengwe viwanda 2,600 lakini tukajikuta viwanda 4,887 vimejengwa, kilikuwa ni kiwango kikubwa sana, hivyo sasa mtumie katazo la serikali kuhamasisha ujenzi wa viwanda vya mifuko rafiki wa mazingi, mrangi mmoja ukigungwa fursa maeneo mengi ya viwanda katika meneo yenu.
Aidha, Jafo pia amewataka wakuu wa mikoa kuhakikisha wanasimamia ipasavyo katazo la mifuko ya platiki katika maeneo yao ili kuiwezesha Tanzania kuungana na nchi zilizokataa kutubia bidhaa hiyo.
“Ikiwa Juni 1 mwaka huu itakuwa mwanzo wa kutotumia mifuko ya plastiki, wakuu wa mikoa mnadhamana, tukiamua kukomesha hili kwa kuhakikisha mnaunga mkono agenda ya serikali ya kupiga matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo imekuwa na madhara ya kiafya na kimazingira.
“ Wakuu wa mikoa mlifanya kazi nzuri sana pale serikali ilipopiga marufuku matumizi ya pombe za viroba, na sasa hali ni nzuri na huwezi kuioana mahali, basi ni imani yangu hata hili la marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki mkisimama kidete litafanyika,” alisema.
Mwezi uliopita, Serikali ilitoa Tamko la kusitisha matumizi ya mifuko ya plastiki hapa nchini ifikapo Juni Mosi 2019, katazo lililolenga kuepusha athari za kiafya na mazingira zinazoendelea kujitokeza kutokana na matumizi ya mifuko hiyo.
Katazo hilo lililotolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa linahusu kupiga marufuku uzalishaji, uingizaji, usafirishaji nje ya nchi, usambazaji, uuzaji na matumizi ya mifuko ya plastiki ya aina zote.
Katika kukabilana na hilo, Serikali imejipanga kuendesha operationi kabambe nchi nzima ya kusakama bidhaa hiyo.
Msako huo utahusisha vyombo vya ulinzi na usalama, kamati za ulinzi na usalama za mikoa, wilaya, mamlaka za serikali za mitaa, Maabara ya Mkemia Mkuu wa serikali, Shirika la Viwango Tanzania(TBS), Mamlaka ya Chakula na dawa(TFDA) Ofisi ya Taifa ya Mashitaka na Viwanja vya Ndege, Bandari, Forodha, Uhamiaji na Usafiri wa Nchi Kavu.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.