Na Nyeneu, P. R - Mjini Babati
Jumuiya ya wanawake wa Chama cha mapinduzi wametakiwa kuhamasisha wanachama wake katika kushiriki michezo kwa kufanya mazoezi ya mara kwa mara ili kusaidia serikali kupunguza ongezeko la magonjwa ya yasiyo ya kuambukiza, hali inayoondoa uwezo wa wazazi wengi kushindwa kuzitunza vyema familia zao.
Ni wito kwa wanawake mkoani Manyara uliotolewa na Katibu Tawala mkoa humo, Bi. Karolina Mthapula baada ya kujumuika na jumuiya hiyo ya Wanawake wa UWT kushiriki katika matembezi yaliyolenga kuhamasisha Wananchi kujitokeza katika kumpokea Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kilele cha mbio za Mwenge wa uhuru ifikapo Oktoba 14 mwaka huu. Matembezi hayo yameishia katika uwanja wa michezo wa Kwaraa na kushiriki katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa uwanja huo ikiwemo kufanya usafi.
Kilele cha mbio za mwenge wa uhuru kinatarajiwa kufanyika mkoani Manyara ambapo mwenge wa uhuru utazimwa katika viwanja vya Kwaraa mjini Babati na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.
Naye mwenyekiti wa Jumuiya ya UWT mkoa wa Manyara Fatuma Tsea, akizungumza baada ya kuhitimisha mbio hizo ameonyesha kufurahishwa na ujenzi wa uwanja wa Kwaraa na kuomba matukio mengine makubwa ya kitaifa kufanyika mkoani hapa kwenye uwanja huo.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.