Tarehe 4. 8. 2023 katika ukumbi namba 83 eneo la ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara kimefanyika kikao cha tathimini ya lishe katika Mkoa wa Manyara.
Kikao hicho kimeongozwa na Mh Razalo Twange Mkuu wa wilaya ya Babati akikaimu na fasi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh Queen Sendiga.
Katika kikao hicho kulikuwa na uwasilishaji wa taarifa ya lishe Mkoa wa Manyara. Afisa lishe Mkoa wa Manyara, Amemueleza mwenye kiti wa kikao hicho kuwa kuna mikakati ambayo imekuwa ikifanywa na wataalamu wa lishe Mkoa wa Manyara.
Mikakati hiyo ikiwa ni usafi wa mazingira ulinzi na uslama kwa watoto pamoja na kilimo cha matumizi ya vyakula vyenye kurutubisha.
Ufugaji wa mifugo midogo midogo sambamba na mikakakti hiyo Afisa lishe Mkoa wa Manyara ameonyesha changamoto zilizopo katika mchakato wakufanikisha suala hilo.
Changamoto hizo zikiwa nipamona na ukosekanaji wa vitendea kazi changamoto ya uhaba wa fedha na ukosekanaji wa uwelewa wakutosha kwa wananchi kuhusu lishe.
Umasikini ambao kwa kiasi kikubwa unachangiwa na vipato duni vya wananchi. Pia idadi ya watoto wanaozaliwa kuwa wengi changamoto ya magonjwa, Ambapo ameeleza kuwa pamoja na changamoto hizo bado kuna mikakati kama Mkoa ilikuweza kufanikisha suala la lishe ambapo mikakati hiyo ni pamoja na kuanzisha bustani mashuleni sambamba na hilo kufanya uchimbaji wa visima kwajili ya umwagiliaji wa bustani hizo.
Mwenyekiti wa kikao hicho (Mkuu wa wilaya ya Babati) Mh Razalo Twange amewataka wataalamu wa lishe wa Mkoa kushirikiana na viongozi wa Halmashauri zote ilikuweza kuhakikisha suala la lishe katika Mkoa wa Manyara linafanikiwa kwa viwango vikubwa zaidi.
Aidha amepokea maoni mbalimbali kutoka kwa wajumbe na wataalamu kutoka Sekta ya elimu na Afya ikiwa nikufanya uboreshaji katika kutekeleza suala la lishe katika Mkoa wa Manyara.
UTEKELEZAJI WA LISHE MKOA WA MANYARA
Kuelimisha wananchi kupitia siku za Afya na lishe za kijiji (SALIKI) kupitia redio wananchi wameendelea kupata elimu kupitia SALIKI.
Hadi kufikia Jun 30 – 2023 utekelezaji ulikuwa ni asilimia 78.6 Ambapo jumla ya vipindi vinne vya redio vimefanyika juu ya Afya na lishe kupitia redio Manyara Fm.
Aidha mpaka Jun 2023 matumizi ya lishe yalikuwa ni TZS 376,702,880.00 (77.59) ya TZS 485,501,810.70 sawa na TZS 1,072 kwa kila mtoto. Ambapo Halmashauri za kiteto DC, Hanang Dc, Babati Tc, na Mbulu Dc, zimetumia fedha zilizopangwa katika kutekeleza Afua za lishe kwa zaidi ya asilimia 84.
Kwa mwaka wa fedha 2022 -2023 baadhi ya vyanzo vya fedha havikuweza kuwezesha utekelezaji wa Afua ya lishe, Aidha kumekuwa na mwendelezo wa utoaji wa elimu ya lishe katika ngazi za wilaya na Halmashauri katika Mkoa wa Manyara.
MATOKEO YA UTEKELEZAJI WA LISHE MKOA WA MANYARA
Katika utoaji wa matokeo hayo ambayo yaliandaliwa kwakufuata vigezo muhimu na vya kitaalamu. Ambapo Halmashauri ya Babati Tc imeshika nafasi ya kwanza katika utekelezaji wa lishe yenye asilimia 16.79.
Ikifuatiwa na Babati Dc yenye asilimia 16.51 Mbulu Dc yenye asilimia 15.26, wilaya ya Simanjiro yenye asilimia 10.86 ikiwa nyuma zaidi ikifuatiwa na Mbulu Tc yenye asilimia 11.63.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.