Maandalizi ya uwanja wa kwaraa uliyo katikati ya mji wa Babati ambao utatumika katika shughuli za kilele cha mbio za Mwenge kitaifa 2023.
upende wa uwanja uko katika hatua ya upandaji wa nyasi ikiwa ni muda wa siku 12 ambapo shuguli ya uwagiliaji wa nyasi hizo unaendelea katika uwanja huwo ambao utatumika katika shughuli hiyo muhimu kitaifa.
Uchimbaji wa Mtalo wakutoa maji kutoka running track na uwanja shughuli hiyo inaendelea na hatua iliyopo nikufuata kwa hatua ya ujenzi wa Mtalo huwo ambapo TANROAD ndio wanao husika na ujenzi wa Mtalo huwo kwajili ya kupitishia maji.
Runing track ina upana wa mita 8 hatua ya base couse inaendelea ilikuweza kufanikisha kutimilika kwake, katika maandalizi ya uwanja wa kwaraa kuna maandalizi yanaendelea katika namna mbili moja ikiwa ni eneo la uwanja wenyewe pili ni katika upande wa majukwaa.
Hatua za maandalizi upande wa majukwaa
Uwanja huwo utakuwa na jumla ya majukwaa matatu (3) ufafanuzi kuhusu ujenzi wa majukwaa hayo nikama ifuatavyo.
Jukwaa la kwanza ujenzi wake unajumuisha mambo yafuatayo Studio kwajili ya urushaji wa matangazo pamoja na chumba cha waamuzi, Pia kuna sehemu ambayo wanakutana wachezaji na waamuzi.
Jukwaa la 2 nala 3 nikwajili ya vyumba vya kubadili nguo sanjari na hivyo katika majukwa hayo matatu kuna jukwaa la kwanza 1 nala 3 hayo nimajukwaa kwajili ya watu mahiri yaani (VIP).
Ambapo jukwaa la 2 hilo litakuwa kwajili ya watu mahiri zaidi yaani (VVIP), wachezaji watakuwa wakitokea jukwaa la watu mahiri zaidi (VVIP) jukwaa la 2.
Sambamba na ujenzi huwo wa majukwaa pia hatua za ujenzi wa vyoo kwajili ya matumizi ya watu watakao ingia uwanja wa kwaraa unaendelea na uko katika hatua zenye kuridhisha, ujenzi kwa ujumla bado unaendelea katika hali ya kuridhisha na unaenda kwa kasi inayotakiwa.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.