Mkuu wa mkoa wa Manyara Mh.Alexanda Mnyeti amefanya ziara katika kijiji cha Naberera Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kutembelea kiwanda cha kusindika Nyama pamoja na Asali ambacho kilifungwa kwa muda wa miaka mitano.Kiwanda hicho kilikuwa kinaendeshwa na kumilikiwa na makampuni mawili ambayo ni (Stich Foundation ) na ( Rotiana social association).
Mmoja wa wakurugenzi wa kiwanda hicho Bi.Mary Mollel alisema kiwanda hicho kilianza kufanya kazi mwaka 2012 na changamoto zilianza mwaka 2013 mwezi Novemba ambapo Muwekezaji aliyekuwepo alikumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo za kisiasa.ufisili wa kiwanda pamoja na mali zilizokuwepo ulitokana na madeni ambayo kampuni ilikuwa inadaiwa na mmoja wa wakurugenzi wa kampuni hiyo pamoja na uvamizi unaofanywa na wananchi ikiwemo kuingiza mifugo katika eneo la kiwanda.
Aidha akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa mwanasheria wa kiwanda Bw.Emmanuel Mrema alisema ni takribani miaka mitano sasa tangu kiwanda hicho kifungwe hii ni kutokana changamoto za umiliki madeni na siasa zisizoleta maendeleo kukwamisha shughuli za uzalishaji ikiwemo kilimo cha mahindi,mtama, maharage pamoja na ufugaji na usindikaji wa nyama .Moja ya hatua ambazo wao wamezichukua ni kuimarisha ulinzi wa eneo la shamba pamoja na kuzuia uvamizi wa wananchi.
Akizungumza katika kikao hicho Mh.Myeti alisema Serikali ya awamu ya tano katika moja ya sera za zake ni “Tanzania ya viwanda” na wao kama Mkoa hawako tayari kuona kiwanda hicho hakifanyi kazi kwani wananchi wa eneo hilo wanategemea ajira pamoja na huduma mbali mbali za kijamii ili kujikwamua kiuchumi.
Moja ya maelekezo aliyoyatoa ni kuitaka serikali ya Wilaya hiyo kufuta hati ya umiliki wa eneo hilo ambapo alisema ” hii hati ya umiliki wa eneo hili haufuati misingi,sheria na kanuni za umiliki wa ardhi Tanzania na hivyo wapewe eneo hili wanapaswa wawekezaji wa ndani au watafute wawekezaji wapya na mchakato wa kukifufuaa kiwanda hicho uanze mara moja na ajira kama ilovyokuwa awali zitolewe kwa wananchi” Alisisitiza
(Kwa Picha mbalimbali angalia Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha)
Imeandikwa na Isabela Joseph (UDSM-Mafunzo kwa Vitendo)
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.