• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

Manyara yapokea vifaa vya kuangalia madini joto kwenye chumvi

Imechapishwa Tarehe: July 1st, 2020

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara leo imepokea chupa sita zenye ujazo wa nusu lita kila moja za Vitendanishi  kwa ajili ya kuangalia madini joto kwenye chumvi kutoka  Taasisi ya Chakula na lishe Tanzania (Tanzania Food and Nutrition Centre - TFNC).

Akikabidhi vitendanishi hivyo Mchunguzi wa Maabara kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Bi.Aldegunda Marundu amesema kuwa wao kama Taasisi wameamua kuusaidia Mkoa wa Manyara ili kuweza kupima madini joto kwenye chumvi na hivyo kupunguza na kuondoa  maradhi yaletwayo na ukosefu wa madini joto kwenye chumvi.

“ Vitendanishi hivi tumevipata kutoka kwa wafadhili wetu ambao ni  TFNC na GAIN na hivyo kuamua kuvisambaza kwenye mikoa mbalimbali hususan Mikoa inayozalisha chumvi kama Manyara” Alisema Bi. Marandu.

Lengo la kufanya usambazaji wa vitendanishi hivyo ni kuwezesha kuendelea kwa zoezi la upimaji wa viwango vya madini jotokwenye chumvi ambao umekuwa ukifanywa na maabara ili kuhakiki viwango vya madini joto yaliyowekwa kwenye chumvi inayotumiwa na jamii. Kwa kufanya hivyo itasaidia kupunguza na hata kuondoa kabisa matatizo yatokanayo na upungufu wa madini joto.

Akipokea Vitendanishi hivyo kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Dkt. Pastory Mahendeka pamoja na kuwashukuru TFNC kwa msaada wao pia aliwaaomba wafadhili hao kuwezesha usimamizi shirikishi katika Mkoa wa Manyara wa kubaini uwepo wa madini joto kwenye chumvi ili kuziwezesha jamii za Mkoa wa Manyara kufahamu umuhimu wa kutumia chumvi yenye madini joto na pia kujua madhara yatokanayo na matumizi ya chumvi isiyo na madini joto.

“Napenda kuwashukuru wafadhili wetu kwa msaada wa vitendanishi hivi, kiukweli katika Mkoa wa Manyara vitendanishi vilituuishia na kwa kupata vitenganishi hivi vitasadia kuendelea na zoezi la upimaji wa madini joto kwenye chumvi” Alisema Dkt.Mahendeka.

Kulingana na Shirika la Afya duniani  matumizi ya chumvi yenye madini joto  katika ngazi ya kaya yanapaswa kuwa zaidi ya asilimia 90 ili kuwezesha kuondokana na madhara yatokanayo na upungufu wa madini joto. Asilimia 65 ya sampuli ya chumvi ya mawe kutoka katika maduka ya reja reja, sokoni na kwenye minada zimebainika kutokuwa na madini joto. Aidha, asilimia 25 ya sampuli za chumvi zilizofungashwa katika pakiti zilizokusanywa kutoka katika maduka ya rejareja hazikuwa na madini joto. Kuhusiana na sampuli za chumvi kutoka ‘supermarkets’, mchanganuo wa kimaabara unaonesha kuwa asilimia 54.6 ya chumvi hizo hazikuwa na madini joto.

changamoto zinazoukabili mpango wa kuchanganya madini joto katika chumvi ni pamoja na uelewa mdogo wa madhara ya upungufu wa madini joto kwa wadau na baadhi ya viongozi wa serikali wenye dhamana ya kutoa maamuzi, upatikanaji endelevu wa fedha na vitendea kazi (rapid salt test kits na vyombo vya usafiri) kwa ajili ya ukaguzi na ufuatiliaji, ukaguzi na uchukuaji wa sampuli za chumvi wa mara kwa mara hasa ukaguzi madhubuti kwa wazalishaji kabla ya chumvi kusambazwa, udhaifu katika utekelezaji wa sheria na kanuni, kukubalika kwa dhana ya matumizi ya chumvi yenye madini joto na uwepo wa wazalishaji wadogo wa chumvi wanaoingiza sokoni (kwa walaji) chumvi isiyo na madini joto.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.