Kuelekea kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Menejimenti ya watumishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara leo tarehe 30 Agosti wametembelea Shule Msingi Kateshi A iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Hanang.
Ambapo Watumishi hao wamepokelewa na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo pamoja na wanafunzi.Shule ya Msingi Kateshi A inawanafunzi wenye mahitaji maalumu 121 wakiwemo wanafunzi wasioona,viziwi na wenye ulemavu wa akili.
Afisa Elimu, Elimu Maalumu amewakaribisha watumishi hao amesema kuwa nifaraja kwake na kwa walimu wa shule ya Msingi Kateshi A kwa watumishi hao kutembelea watoto wenye uhitaji maalumu. Pia ameshukuru kwa ushirikiano wanaoupata kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ikiwa ni pamojana na uboreshaji wa miundo mbinu ya elimu katika Shule ya Msingi Kateshi A.
Aidha Dokta Damasi Kayela kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Manyara ameeleza kuwa ujio wa watumishi hao kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa nikuleta mahusiano mazuri kati yao na jamii. Ameeleza juu ya matarajio makubwa kwa wanafunzi hao wenye mahitaji maalumu, amewatakia mafanikio katika masomo yao. Sambamba na hayo ametoa Kadi 96 za Bima ya Afya na taulo za kike (SODO) kwa wanafunzi wa kike wenye uhitaji maalumu.
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kateshi A amewashukuru watumishi hao kutoka katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa jamii kuwapa nafasi ya kupata elimu watoto wenye mahitaji muhimu nakuto wanyima fursa ya kielimu.
Kwa niaba ya wanafunzi wenzake Ernest Maiko amewashukuru watumishi hao kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kutoa Bima ya Afya ambazo zitawasaidia kwa matibabu yao ya kila siku.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.