• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

MIRADI 44 YA ZAIDI YA BILLION 8 KUZINDULIWA NA MWENGE WA UHURU MANYARA

Imechapishwa Tarehe: June 13th, 2019

Mwenge wa uhuru umewasili mkoani manyara na kupokelewa katika kijiji cha aicho halmashaur ya mji wa mbulu ambapo ukiwa mkoani hapo utatembelea na kukagua, kuzindua na kuona miradi 44 yenye thamani ya zaidi ya bilioni nane katika halmashaur Saba za mkoa huo.  Halmashaur zitakazopitiwa na mwenge ikiwa ni pamoja na kukaguliwa na kuweka jiwe la msingi ni Halmashauri ya mji wa mbulu, Halmashauri ya wilaya ya mbulu, Halmashauri ya hanang, halmashauri ya babati mji, halmashauri ya wilaya ya babati, halmashauri ya kiteto pamoja na halmashauri ya kiteto.

Akipokea mwenge wa uhuru kutoka mkoa wa Arusha makabidhiano hayo yalifanyika katika kijiji cha Aicho kilichopo wilaya ya mbulu mkoani humo mkuu wa mkoa wa manyara Alexander  Mnyeti alisema mwenge wa uhuru ni moja ya alama ya Uhuru umoja na utaifa wa watanzania hivyo kwa kuzingatia hilo wananchi wa Manyara wanatambua umuhim wa mbio za mwenge wa uhuru kuwa ni chachu ya kuleta maendeleo na kuleta matumaini pale ambapo hapana matumaini upendo pale ambapo pana chuki na kuleta heshima sehemu palipojaa dharau.


Kati ya miradi 44 inayotarajiwa kuzinduliwa na mwenge wa uhuru ni pamoja na kuweka jiwe la msingi katika miradi 16 yenye thamani ya zaidi ya billion 3,kuzindua miradi 14 yenye thaman ya zaidi ya billion 2 pamoja nankuzindua miradi mbalimbali iliyogharimu zaidi ya million 600,kukagua miradi 10 iliyogharimu zaid ya billion 1 ambapo alieleza katika miradi hiyo nguvu za wananchi ni zaidi ya million 344 na serikali kuu ni jumla ya million 5899  na mamlaka za seikali za mitaa ni jumla ya million 211 na wahisani ni zaidi ya  billion 1.

Aidha Mnyeti alisema wananchi wa mkoa wa manyara wameopokea vizuri mwenge wa uhuru na watatekeza kwa vitendo  kauli mbiu yake inayoeleza kuwa "maji ni haki ya kila mtu tuunze vyanzo vyake  na tukumbuke kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa"hakika ujumbe huo umesadifu na umelenga kuwafahamisha na kuwahamasisha wananchi kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji na kuwakumbusha kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa.

Ukiwa mkoani humo katika wilaya ya mbulu Mwenge ulifanikiwa kuzindua jumla miradi saba ambapo pia ulifanikiwa kuzindua mradi wa maji katika kata ya Barigish kijiji cha Arri  Bans wenye thamani ya Tsh million 399 unaotarajia kuwakomboa na adha ya maji zaidi ya wakazi wapatao 4597 wa kata hiyo.


Akizungumza mara baada ya kuzinduliwa kwa mradi huo Bw. Samweli John mkazi wa kijiji cha Arri Bans alieleza kuwa ni wakati wa wananchi kuwa wazalendo kwa kulinda miundombinu ya maji hiyo huku akisisitiza kuwa awali walikuwa wakitumia maji ambayo siyo safi hivyo wanaishukuru serikali kwa kusikia kilio chao cha muda mrefu.

Akizungumza na wananchi wa mkoa wa manyara kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Mzee Mkongeya Alli alisema kuwa ni takribani miaka 20 imefika toka kifo cha baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hivyo katika kimuenzi hatoacha kufanya kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni pamoja na kupambana na adui Ujinga, Maradhi na Umasikini ikiwa ni pamoja kuwahamasisha wananchi kulipa kodi ili kuongeza pato la Taifa.

Aidha Mzee Mkongea alisema kuwa kwa kutambua umuhimu wa maji ilani  ya Uchaguzi ya chama cha mapinduzi CCM ya mwaka  2015/2020 ni kuhakikisha ifikapo 2020 wananchi wote wanaoishi vijijini wanapata maji safi na salama kwa asilimia 85.

"Hivyo katika wa ilani hiyo kuanzia mwaka 2006 hadi mwaka 2018 kwa upande wa vijijini miradi ipatayo 1659 imeweza kukamilishwa kwa wakati lakini bado serikali inasera za kimkakati za uchimbaji wa visima vya maji virefu na vifupi ambavyo  vimegharimu billion 14 " Alisema Mzee Mkongea.

Pia akawataka wananchi kutunza na kulinda vyanzo vya maji ili viweze kudumu kwa vizazi vya sasa na vizazi vijavyo ikiwa ni pamoja na kuacha kufanya shughuli za binadamu pembezo mwa vyanzo vya maji ikiwa ni kulima na kuchunga mifugo. 

(Kwa picha mbalimbali  angalia sehemu ya  Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha)

Imeandikwa na:Haji A.Msovu


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.