• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

Mkirikiti awataka Wakurugenzi Manyara kutoa fedhaa zilizotengwa kwa ajili ya lishe

Imechapishwa Tarehe: July 24th, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Joseph Joseph Mkirikiti (mstari wa mbele katikati) akiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kikao cha tathimini ya lishe Mkoa 24 Julai,2020.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Joseph Joseph Mkirikiti amewataka Wakurugenzi wote wa Halmashauri za Mkoa wa Manyara kuhakikisha fedha zilitengwa kwa ajili lishe zinawafikia walengwa na kutumika ipasavyo kama miongozo inavyoelekeza. Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo  leo Ijumaa 23 Julai alipokuwa akifungua na kuendesha kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara kilichozungumzia juu ya tathimini ya nusu mwaka ya mkataba wa lishe kwa ngazi ya Mkoa na Halmashauri zote za Mkoa wa Manyara.

 Wakitoa malalamiko yao Maafisa lishe waliohudhuria katika kikao hicho walisema wanashindwa kutekeleza majukumu yao kwa sababu ya changamoto ya kutokupewa fedha za kuwahakikisha wanaondoa hali ya udumavu.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Joseph Joseph Mkirikiti akifungua kikao cha tathimini ya lishe Mkoa 24 Julai,2020.

Baadhi ya wajumbe waliohudhuria  kikao cha tathimini ya lishe Mkoa kilichoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara 24 Julai,2020.

Akijibu hoja hiyo Mkuu wa Mkoa aliwaagiza maafisa wanaoshughulikia mipango na bajeti ngazi ya Halmashauri hasa Maafisa mipango na makatibu wa afya wa Halmashauri waache maafisa lishe wahusike moja kwa moja katika kupanga afua za lishe ndani ya mfumo ulioboreshwa wa PlanRep maana kumekuwepo na tabia ya kupunguza afua bila kuzingatia weledi na ndo maana afua hizo hazileti tija.

Akifungua kikao hicho Mkuu wa Mkoa aliwataka wajumbe waliohudhuria kuhakikisha wanawakumbusha wajumbe wa kamati zote kuanzia ngazi ya Mkoa,Halmashauri,Kata na Vijiji pamoja na viongozi wote kutoa kipaumbele kwa masuala ya lishe ili kuweza kupunguza kiwango cha udumavu katika Mkoa wa Manyara.

“Watoto 36 kati ya 100 wamedumaa Mkoani kwetu na hivyo hawana uwezo wa kufundishika na hata kuleta tija katika kuinua uchumi wa Taifa na badala yake gharama kubwa hutumika kuwatunza, kwa hiyo nawataka wahusika wote kuhakikisha tunapunguza kiwango cha udumavu katika Mkoa wa Manyara” Alisema Mhe.Mkirikiti.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Joseph Joseph Mkirikiti akiendesha kikao cha tathimini ya lishe Mkoa 24 Julai,2020.

Baadhi ya wajumbe waliohudhuria  kikao cha tathimini ya lishe Mkoa kilichoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara 24 Julai,2020.

Vilevile alizitaka Halmashauri kuhakikisha masuala ya lishe yafanywe kama agenda ya kudumu kuanzia ngazi ya mkoa hadi kijiji na mtaa na ikiwezekana lipelekwe hadi Makanisani na Misikitini kwa waumini wasiokuwa na lishe nzuri hata kusikiliza mahubiri na kuelewa na vigumu.

Afisa Lishe Mkoa wa Manyara Bwana Mabula Masunga akitoa mada wa wajumbe wa  kikao cha tathimini ya lishe Mkoa 24 Julai,2020.

Baadhi ya wajumbe waliohudhuria  kikao cha tathimini ya lishe Mkoa kilichoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara 24 Julai,2020.

Katika Kikao hicho Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa aliwashukuru wadau mbalimbali wakiwemo GAIN ambao wamekuwa nguzo kubwa katika kuimarisha elimu ya matumizi ya chumvi yenye madini joto na Shirika la lisshe la kimataifa la “Nutrition International” wanaofadhili Mkoa wa Manyara katika uchakataji madini joto kwenye chumvi.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Joseph Joseph Mkirikiti akiendesha kikao cha tathimini ya lishe Mkoa 24 Julai,2020.

Baadhi ya wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Manyara waliohudhuria  kikao cha tathimini ya lishe Mkoa kilichoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara 24 Julai,2020.

Katika Kikao hicho Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto imepewa zawadi ya cheti kwa kuwa wa kwanza katika kutekeleza mpango wa lishe ikifuatiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Joseph Joseph Mkirikiti (kulia) akimkabidhi cheti cha ushindi Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Kanali Patrick Norbert Songea katika  kikao cha tathimini ya lishe Mkoa 24 Julai,2020.

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Kanali Patrick Norbert Songea (kulia) akiwa na Maafisa Lishe wa Wilaya hiyo baada ya kukabidhiwa cheti cha ushindi katika  kikao cha tathimini ya lishe Mkoa 24 Julai,2020.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Joseph Joseph Mkirikiti (kulia) akimkabidhi cheti cha ushindi Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbulu katika  kikao cha tathimini ya lishe Mkoa 24 Julai,2020.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbulu Bi. Sarah Sanga (kulia) akiwa na Maafisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu baada ya kukabidhiwa cheti cha ushindi katika  kikao cha tathimini ya lishe Mkoa 24 Julai,2020.

Hiki ni kikao cha nusu mwaka cha lishe na Mkoa wa Manyara umekuwa ukitekeleza Nkataba wa lishe kila mwaka kwa utaratibu ulijiwekea ukishirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI ili kutathmini ulivyotekeleza afua mbalimbali kulingana na viashiria na vigezo vilivyowekwa wakati wa kutia saini mkataba wa lishe.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Joseph Joseph Mkirikiti akiendesha kikao cha tathimini ya lishe Mkoa 24 Julai,2020.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Joseph Joseph Mkirikiti (mstari wa mbele katikati) akiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kikao cha tathimini ya lishe Mkoa 24 Julai,2020.


Imeandikwa Na:Haji A.Msovu (Afisa Habari Mkoa wa Manyara)

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.