Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joseph Mkirikiti amewashauri wawekezaji kutoka Tanzania na nje ya Tanzania kuja kuwekeza mkoani Manyara kutokana na uwepo wa fursa mbalimbali za uwekezaji zipatikanazo mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo leo alipokuwa akifungua kikao cha Kamati ya ushauri wa Mkoa (RCC) kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkuu wa Mkoa kwa kusema kuwa Pamoja na Mkoa huo kuwa ni Mkoa wa tatu kwa ukubwa nchini kuna rasilimali za kutosha katika sekta za Madini,Utalii,Mifugo,Uvuvi, Kilimo hivyo kuwataka wajumbe wa kikao hicho kujipima ili kujua jinsi gani ya kutafuta wawekezaji kwenye Mkoa huo ili kuleta maendeleo katika Mkoa wa Manyara.
“Ni vizuri tukajadiliana na kila mmoja wetu akajipima ili tukauweka Mkoa wetu kuwa katika namna bora Zaidi” Alisema Mhe.Mkirikiti.
Vilevile Mhe. Mkuu wa Mkoa aliwataka viongozi kujenga mahusiano mazuri ya kazi kati Viongozi na wawakilishi wa wananchi ili kujua matatizo mbalimbali yanayowakabili kwa lengo la kuwaletea maendeleo katika maeneo mbalimbali.
Mkuu huyo wa Mkoa alitaka wajumbe waliohudhuria kikao hicho kujadiliana kwa kina katika kila sekta kuanzia kwenye Mifugo,Kilimo, uvuvi ili tija kwa wananchi wa Mkoa wa Manyara.
“Niwaombe sana wajumbe tutumie kikao hiki vizuru, tujadiliane kwa uwazi, bila shaka nina Imani tukiangalia yale yaliyojadiliwa na wenzetu katika vikao vilivyopita tukaweka nay a kwetu Pamoja na kuweka dira yeti bila shaka tutafanikiwa kama Mkoa” Alisisitiza Mhe.Mkirikiti.
Akizungumzia njia mbalimbali za kutatua changamomoto zilizopo katika Mkoa wa Manyara Mhe. Mkirikiti aliwata wajumbe kujadiliana kwa kina juu ya changamoto mbalimbali zikiwemo za migogoro ya ardhi Pamoja na changamoto za zizopo katika Madini, Kilimo,Utalii, mifugo, na sekta ya Elimu na kuzitafutia suluhisho la kudumu ili wananchi waone jinsi Serikali yao inavyowatumikia kwa moyo mmoja.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.