Wadau wa Afya wa mkoa wa Manyara wamekutana tareha 27 na 28 mwezi wa 8 mwaka 2018 katika Halmashauri ya wilaya ya Hanang kujadili taarifa mbalimbali za kiafya ,changamoto,mafanikio, malengo ya kuboresha afya na kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma bora za kiafya.
Akifungua kikao hicho Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mh. Joseph Mkirikiti alisema alitoa shukrani kwa wadau wote walioshiriki, taasisi na mashirika binafsi na amefurahishwa na jinsi ambavyo idara ya afya na vituo vyake jinsi ilivyopanga mikakati ya kimaendeleo na malengo mahususi ya kuboresha afya katika mkoa wetu ili hali tunapitia changamoto mbalimbali lakini anatumai ushirikiano wetu na umoja wetu baina ya serikali, mashirika na wadau tunaweza kufikia lengo na kuboresha huduma za afya kwa wananchi kwa wakati alisisitiza”
Akisoma taarifa ya mradi wa shirika la msaada la Watu wa Marekani (USAID) BORESHA AFYA meneja wa kanda ya Kaskazini Dkt. Leo Haule amesema kuwa serikali ya Mkoa wa Manyara kwa ushirikiano wa mradi wa USAID BORESHA AFYA wamefanikiwa kupiga hatua katika huduma za upimaji wa VVU, kutoa dawa za ARV na dawa za kufubaza makali ya virusi vya ukimwi zinapatikana na kuwafikia wananchi kwa wakati.
Aidha alisema kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita kati ya mwezi april 2017 hadi juni 2018 kwa ufadhili uliotolewa na shirika la msaada la kimarekani (USAID) ambapo jumla ya wananchi 184,802 walipatiwa huduma za upimaji pamoja na ushauri nasaha katika vituo vinavyofikiwa na mtu mmojamoja. Kati ya hao jumla ya wananchi 3,114 walipatikana na maambukizi ya VVU ambao ni sawa na asilimia1.7 halikadhalika wananchi 2050 walianzishiwa dawa za kufubaza makali ya VVU ambao ni sawa na asilimia 66 ya wananchi wote waliokutwa na maambukizi.
Pia kwa kipindi cha toka April 2017 hadi jun2018 jumla ya wananchi 2243 walipimwa uwingi wa VVU katika damu,katiyao 1850 ambao ni sawa na asilimia 82 walikutwa na virusi vilivyofubaa. Vilevile tangu july 2017 hadi june 2018 USAID BORESHA AFYA na kamati za afya za Halmashauri zote saba na kamati za afya za mkoa zimewezesha asilimia 90 ya wananchi wote wanapata huduma za tiba na matunzo kufanyiwa uchunguzi wa kifua kikuu, ambapo jumla ya wagonjwa 2,948 wa kifua kuu waliweza kuibuliwa na kupatiwa matibabu, kati ya hao 360 walipatikana na maambukizi ya VVU ambao ni sawa na asilimia12 .Pia jumla ya wananchi 315 walikutwa na kifua kikuu na VVU kwa pamoja na kuanzishiwa dawa za kufubaza makali ya VVU ambao ni sawa na asilimia 88.
Vilevile idadi ya wajawazito wapatao 31,431 walipimwa VVU na kati ya 326 walikutwa na maambukizi ikiwa ni sawa na asilimia moja ,katiyao 305 walianzishiwa dawa ya kufubaza makali ya VVU ambao ni sawa na asilimia 94 ya wajawazito wote waliokutwa na maambukizi. Shirika la Elizabeth Glaser linalopambana na VVU/UKIMWI kwa watoto (EGPAF) kwa ushirikiano na serikali na Engender health linatekeleza mradi wa USAID BORESHA AFYA katika mikoa sita ya kati na kaskazini mwa Tanzania ukiwamo Manyara.
USAID BORESHA AFYA unatekeleza afua zinazochangia juhudi za serikali kutokomeza maambukizi mapya ya VVU ifikapo mwaka 2030.Hili linafanyika kwa kuweka juhudi kufikia malengo ya kitaifa ya 90, 90, 90 yaani kupima asilimia 90 ya watu wote ili wajue hali zao,kuanzishiwa dawa za kufubaza makali ya VVU asilimia 90 ya waliokutwa na maambukizi ya VVU na kuhakikisha asilimia 90 ya wanaotumia dawa wanakuwa na virusi vilivyofubazwa.
Hadi sasa USAID BORESHA AFYA inatekeleza afua za upimaji na matibabu kwenye vituo vya tiba 38 katika Halmashauri saba za mkoa wa Manyara ambapo katika mwaka wa fedha wa 2017/2018 Halmashauri hizo zilipatiwa jumla ya Tsh billion 1 na million 150 ili kutekeleza za afua za upimaji na matibabu ya VVU/UKIMWI,uzazi wa mpango na kifua kikuu.
Pamoja na uzinduzi huo kutakuwa na kampeni ya upimaji virusi vya ukimwi siku ya tarehe 29 katika viwanja vya shule ya Msingi Katesh wilaya ya Hanang ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni” furahayangu,pima,jitambue,ishi”
Kwa Picha na Video mbalimbali angalia Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha
Imeandikwa Na: Isabela Joseph (UDSM- Mafunzo kwa Vitendo)
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.