Na Nyeneu, P. R - Mjini Babati
Mradi wa BOOST ni mradi wa kuimarisha na kuboresha elimu ya awali na msingi hapa nchini ambao una thamani ya Tsh Trilioni 1.15. Mradi huu unatekelezwa nchini kwa muda miaka 5 hivyo kukamilika mwaka 2025/2026 na umelenga kunufaisha Halmashauri zote 184 nchini hususani katika kuboresha miundombinu ya elimu kwa Madarasa ya awali na Msingi.
Kupitia Mradi huo, Mkoa wa Manyara umepatiwa jumla ya Shilingi 6,417,100,000 kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya za Msingi 08, vyumba vya madarasa 72 vya Shule za Msingi, vyumba vya Madarasa ya mfano ya Elimu ya Awali 14, chumba cha darasa 01 kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum, matundu ya vyoo 90, mabweni 02, nyumba za walimu 02 (2 in 1), na ukarabati wa Shule ya Msingi Kongwe 01.
Aidha, mradi huu ni wa Lipa kwa Matokeo (P for R), hivyo, inaelekezwa kukamilisha kwa wakati na kwa kufuata taratibu zote zilizowekwa ili Serikali iendelee kupata fedha za ujenzi kupitia Mradi wa BOOST.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.