• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

RAIS MAGUFULI ATOA MAAGIZO KWA WIZARA YA MADINI NA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

Imechapishwa Tarehe: January 23rd, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewaagiza viongozi wa Wazira ya Madini na Wizara ya Fedha na Mpango kujadiliana na kukubaliana na wadau wa madini kuhusu utaratibu mzuri utakaowezesha kuongezeka kwa mapato yatokanayo na madini yote yanayozalishwa hapa nchini ikiwemo kupendekeza viwango vya tozo za kodi na ushuru vitakavyowavutia wadau kulipa tozo hizo badala ya kukwepa.

Mhe. Rais Magufuli ametoa maagizo hayo tarehe 22 Januari, 2019 katika kituo cha kimataifa cha mikutano cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam baada ya kupokea maoni ya wachimbaji wadogo, wafanyabiashara na wadau wengine wa sekta ya madini wanaokutana kwa siku mbili kituo hapo kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yahusuyo madini.

Katika maoni yao wadau hao wa madini wamemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa tozo kubwa na nyingi zilizowekwa katika madini hasa dhahabu zimesababisha wachimbaji wadogo na kati na wafanyabiashara wengi kukwepa kuuza madini yao katika utaratibu rasmi, hali inayosababisha zaidi ya asilimia 90 ya dhahabu inayozalishwa hapa nchini kutoroshwa na hivyo kusababisha Serikali kukosa mapato.

Wamezitaja tozo hizo kuwa ni kodi ya ongezeko la thamani (VAT) inayotozwa kwa asilimia 18, kodi ya zuio ya asilimia 5, kodi ya ukaguzi ya asilimia 1, ushuru wa huduma wa asilimia 0.3, mrahaba wa asilimia 6 na hivyo kufanya jumla ya tozo kuwa asilimia 30.3, na baadaye wanatozwa kodi ya kampuni kwa mwaka ambayo ni asilimia 30 ya faida.

Aidha, wadau hao wameomba wataalamu na viongozi wa madini wawe karibu na wachimbaji ili kujua uhalisia uchimbaji na biashara yake, kutafuta suluhisho la madini yaliyozuiliwa kusafirishwa nje ya nchi kutokana na kukosekana kwa mitambo ya kuchakatia, kupunguza gharama za leseni, kuanzisha vituo vya masoko ya madini, kupata bei elekezi ya madini ya viwanda na ujenzi na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kununua dhahabu.

Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali itakuwa tayari kufanyia kazi mapendekezo ya wadau hao yenye lengo la kuongeza ukusanyaji wa mapato ikiwemo kupeleka Bungeni marekebisho ya sheria zinazohusu tozo za madini ili nchi iweze kunufaika na rasilimali hiyo, tofauti na sasa ambapo utoroshaji wa madini, ukwepaji wa kodi na wizi vinasababisha madini ya Tanzania kuzinufaisha nchi nyingine.

Amemtaka Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko kuhakikisha anachukua hatua za haraka za kufanya mabadiliko katika maeneo yote yaliyoonesha udhaifu ndani ya wizara hiyo ikiwemo kuwaondoa viongozi na wataalamu ambao wamekuwa chanzo cha upotevu wa mapato ya Serikali, kutafuta wawekezaji watakaojenga viwanda vya kuchenjua na kuchakata madini na kuanzisha vituo vya kuuzia madini.

Mhe. Rais Magufuli ametoa siku 30 kwa Waziri Biteko kuhakikisha ukuta wa kuzunguka madini ya Tanzanite wa Mererani unawekewa kamera za ulinzi na vifaa vya ukaguzi kwa wanaoingia na kutoka katika eneo hilo, pamoja na kuondoa sharti linalowataka vijana wenye ajira ndio waruhusiwe kuingia, hali iliyosababisha kuwepo malalamiko kuwa linasababisha vijana wasio na ajira kuingia kwa kuruka ukuta na kuwepo uhaba wa wachimbaji migodini.

Pia amemuagiza Waziri Biteko kuhakikisha maeneo yote ya madini ambayo yanashikiliwa na watu bila kufanyiwa kazi yananyang’anywa ili wapewe wachimbaji ambao wapo tayari kuchimba madini, kwa kutoa kipaumbele kwa wachimbaji wadogo na wa kati ambao wametajwa kufikia Milioni 6.

Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko, Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango, Baadhi ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Wakuu, viongozi wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Viongozi wa Dini na viongozi wa vyama vya siasa.

 

 

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

22 Januari, 2019

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.