Na, Ruth Kyelula, Manyara RS
Katibu Tawala Mkoa wa Manyara, Bi. Maryam Muhaji, alisema kuwa Mkoa umelenga kushirikiana na shirika la EGPAF (Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation) ifikapo mwaka 2028 kusiwepo na mtoto anaezaliwa na virusi vya UKIMWI.Na kuongeza kuwa suala hilo linawezekana.
Aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wa siku moja wa kutathimini maendeleo ya mkakati wa kuharakisha matokeo ya mradi wa USAID afya yangu Northen 2024/25, uliofanyika mjini Babati Septemba 22, 2025 na wadau mbalimbali kama USAID Afya yangu, Baraza la watu wanaoishi na UKIMWI, Wadau wanaojishughulisha na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu (ACHIEVE), Shirika la Posta, TACAIDS, Halmashauri saba za mkoa na Secretariet ya Mkoa walishiriki.
“Najua kwenye program hizi mmetusaidia sana hasa upimaji wa HIV, masuala ya kifua kikuu lakini kubwa zaidi masuala ya watumishi.Mimi ningeomba sana sana haya masuala bado tunahitaji msaada toka kwenu,bado watumishi hawatoshelezi,mkoa wa Manyara ni mkoa ambao umebahatika mno kwa kupata proramu nyingi ni miongoni mwa mikoa michache Tanzania ambayo mmeiangalia kwa jicho la kipekee, mimi niseme nawashukuruni sana lakini nitoe msisitizo kwenye hili, bado mkoa wa Manyara tunatakiwa tupate watumishi zaidi, tupate sapoti ya upimaji wa HIV,lakini pia suala zima la kifua kikuu, na upimaji wa sampuli, tunaomba kama wadau wetu tuwe pamoja kwenye hili.” Alisema Muhaji.
Aliendelea kusema kuwa, kwa sapoti ya Serikali na wadau anaamini watafikia lengo hata kabla ya mwaka 2028, na wanaweza. Aidha ameiahidi EGPAF kuwa, yale yote ambayo wamewakabidhi mkoa wayafanyie kazi na wayasimamie, wataenda kuyasimamia.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.