Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi itakayo zinduliwa na kutembelewa na Mwenge wa Uhuru 2023 katika Halmashauri ya Mji wa Babati na Halmashauri ya Babati Wilaya. Katika ziara hiyo, Mhe. Mkuu wa Mkoa ameambatana na Katibu Tawala Mkoa Bi. Karolina Mthapula, kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange.
Mhe. Sendiga mefanya ukaguzi wa eneo lakupokea Mwenge Uhuru 2023 lililopo kijiji cha kiongozi Kata ya Maisaka katika Halmashauri ya Mji wa Babati ambapo amewataka viongozi kutoa hamasa ilikufanikisha mapokezi ya Mwenge katika eneo hilo. Pia ametembelea mradi wa maji unaosimamiwa na kutekelezwa na Wakala wa maji na usafi wa mazingira Vijijini (RUWASA) katika mtaa wa Maisaka Kati Kata ya Maisaka ambapo ametoa maelekezo kuhusu mradi huo na kusisitiza usafi.
Vilevile Mhe. Mkuu wa Mkoa ametembelea mradi wa utunzaji mazingira uliyopo mtaa wa Maisaka Kati Kata ya Maisaka sambamba na hilo amefanya ukaguzi wa Klabu za kupinga Rushwa katika shule ya Sekondari Kwaraa iliyopo katika Kata ya Babati. Nao wanafunzi wa Klabu hiyo katika shule ya Kwaraa, wameonyesha igizo fupi kuhusu upingaji wa rushwa, aidha Mhe. RC amesisitiza juu ya utunzaji wa mazingira katika shule hiyo.
Pia amefanya ukaguzi wa mradi wa karavati katika kijiji cha Mutuka Kata ya Mutuka na kutoa maelekezo kuhusu mradi huo. Vilevile amefanya ukaguzi wa mradi wa madarasa matatu katika shule ya msingi Hangoni iliyopo Kata ya Babati zote zikiwa katika Halmashauri ya Mji wa Babati. Mhe. Mkuu wa Mkoa amewapongeza kwa kutekeleza mradi huo vizuri huku akiwataka kukamilisha miradi yote kwa wakati.
Aidha, Mhe. Sendiga amefanya ukaguzi wa Daraja la Bacho lililopo Kata ya Ayalagaya Kijiji cha Haysam katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati. Pia, amefanya ukaguzi katika shule ya msingi Masabeda iliyopo Kata ya Bashinet Kijiji cha Masabeda. Mkuu wa Mkoa amehitimisha ziara yake na kufanya ukaguzi wa mradi wa maji uliokuwa ukitekelezwa na RUWASA katika Kata ya Nar kijiji cha Nar ambapo amefurahishwa na mradi huo utakao ondoa tatizo la maji katika kijiji hicho.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.