• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

RUWASA Kumaliza shida ya Maji Manyara

Imechapishwa Tarehe: February 6th, 2021

Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) imetenga zaidi ya  Shilingi Bilioni tisa kwa ajili ya kukamilisha miradi ya maji Mkoani Manyara ambapo kwa kila Mkoa umetenga Wilaya  Shilingi Bilioni 1,366,865 na kwa Wilaya ya Simanjiro  imepanga kutekeleza miradi sita iliyopo Wilayani humo ili kuhakikisha wananchi wa Wilaya hiyo wanaepukana na kero za kutafuta maji be kwa kutembea umbali mrefu.

Hayo yamesemwa jana  na Meneja wa RUWASA Mkoa wa Manyara Mhandisi Wolta Kirita wakati wa ukaguzi wa miradi ya Maji uliofanywa na Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo, Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joseph Mkirikiti na Kamati ya siasa Mkoa wa Manyara Wilayani Simanjiro katika kuhakikisha kauli ya Mhe.Rais John Pombe Magufuli ya kumtua Mwanamke ndoo kichwani inatimia kwa kuhakikisha wananchi hawatembei umbali mrefu kutafuta maji.

"Mheshimiwa Waziri Mkuu Mstaafu kwa kipindi cha mwezi Oktoba 2019 hadi 2021 RUWASA imejipanga kuhakikisha inamalizia miradi sita ya maji iliyopo katika Vijiji vya Oljoro namba 5,Narakauo,Longswan-Terrat,Komolo,Shambai-Kilombero na Emboreet ambapo tunatarajia kuwanufaisha wakazi 15,246 watanufaika na  mradi huu kwani tutajenga vituo 47 vya kuchotea maji"Alisema Mhandisi Kirita.

Pamoja na mradi huo wa Longswan Mheshimiwa Waziri Mkuu Mstaafu na Viongozi alioambatana nao walitembelea mradi mkubwa wa Ruvu-Remit unaogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 40  unaondelea kunajengwa katika mji wa Orkesumet.Mara baada ya kukamilika kwa mradi huo wananchi wa Simanjiro,Mirerani,Kiteto,na baadhi ya Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro pia watanufaika na maji kwa mradi huo una uwezo wa kuhudumia watu wengi kuliko idadi ya wananchi waliopo Wilayani humo.
Pia Viongozi hao walitembelea mradi mwingine wa maji wa Londrekes.

Pamoja na kuridhishwa na miradi hiyo mara baada ya Viongozi hao kukagua na kujionea maendeleo ya miradi hiyo Viongozi hao waliwataka Viongozi katika ngazi za Vijiji na Kata wawe wasimamizi wakubwa juu wa wananchi wanaohujumu miundombinu ya maji inayofanywa katika maeneo yao ya utawala.


"Kiukweli sisi kama Viongozi tumekagua miradi hii na tumeridhika nayo ila napenda kuwaambia Viongozi wenzangu katika ngazi za Vijiji na Kata kuhakikisha mnalinda miundombinu hii ili isiharibiwe kwani Serikali inatumia fedha nyingi sana kuwekeza katika miradi ya maendeleo ili wananchi wake wapate huduma nzuri, sasa hakikisheni mnawabaini  wote wanaohujumu miundombinu ya maji na mingine na kuwachukulia hatua kali za kusheria" Mhe. Joseph Mkirikiti.


Kwa upande wake Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Pinda alifurahishwa na jinsi RUWASA wanavyojitahidi kuhakikisha wanapelea huduma za maji kila kona na kuwataka wakala hao kuwa kama Shirika la Umeme linavyopeleka umeme kila kona.


"RUWASA pamoja na kazi nzuri mnayofanya mnatakiwa kuhakikisha mnawafikishia maji wananchi kila mahali kama wanavyofanya Tanesco katika umeme". Alisisitiza Mhe.Pinda.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara na kamati ya Siasa Mkoa  wanaendelea na ziara yao ya kukagua miradi ya maji inayotekelezwa na wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) katika Wilaya zote za Mkoa huo ili kuhakikisha wananchi wa Manyara wanaepukana na kero za kutafuta maji kwa kutembea umbali mrefu.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.