Wakala wa Maji Vijijini RUWASA katika Wilaya ya Mbulu imepanga kutumia zaidi ya Bilioni tatu kutekeleza miradi ya maji ili kuondoa kero za upatikanaji wa maji katika wilaya hiyo.
Hayo yamesemwa leo na Meneja wa RUWASA wilaya ya Mbulu Mhandisi Philimon Qamara alipokuwa akisoma taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara alipokuwa katika ziara ya kukagua miradi ya maji katika Wilaya ya Mbulu.
“Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa RUWASA Wilaya ya Mbulu imepewa shilingi Bilioni 1.3 fedha zilizokusudiwa kutekeleza miradi mitatu ya maji katika wilaya yetu hususani katika Kijiji cha Maghang,Hyderer na Dongobesh” Alisema Mhandisi Qamara.
Pamoja na ujenzi wa vituo hivyo vya maji kuendelea ili kuhakikisha maji yanapatikana lakini kuna changamoto ya kupata nguvu kazi ya uchimbaji wa mitaro.
“Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Pamoja na jitahidi kuwalipa vibarua wanaochimba mitaro kwa shilingi 1000 kwa mita moja lakini imekuwa ngumu kuwapata kwa madai kuwa hali ya ardhi ni ngumu” Alisema Mhandisi Philimon Qamara.
Mara baada ya kusomewa taarifa hiyo Mkuu wa Mkoa amefurahishwa na jinsi ya RUWASA Wilayani Mbulu inavyojitahidi kuhakikisha huduma ya maji inawafikia kila mahali ili wasihangaike kutembea umbali mrefu kutafuta kwani Mheshimiwa Rais anataka kuhakikisha Mwanamke anatuliwa ndoo kichwani kwa kumuondelea adha ya kupata maji na pia kuwataka viongozi katika maeneo hayo kuhamasisha vijana kuchimba mitaro ili utandazaji wa mabomba uanze mara moja.
“Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya hakikisheni mnawahamasisha vijana wachimbe mitaro ili wananchi wapate maji kuanzia mwishini mwa mwezi wa kumi na hao vijana ni bora wakafanya kazi za kuchimba mitaro na kulipwa kuliko kukaa vijiweni” Alisema Mhe.Mkirikiti.
Mara baada ya kutembelea miradi ya maji Mhe.Mkuu wa Mkoa pia alifanya ziara ya kutembelea katika majengo ya Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya Mbulu na Hospitali ya Wilaya yanayojengwa katika Mji wa Dongobesh na kuwapongeza wakandarasi kwa kazi nzuri wanaiyoifanya.
Mhe.Mkirikiti amemtaka Mkurgenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mbulu na Wataalamu wake kuhakikisha wanapanga matumizi mazuri ya Ofisi hizo ikiwemo kuhakikisha wananchi wanapata huduma nzuri na pia kulifanya jingo hilo liwe sehemu ya kuongeza mapato ya Halmashauri kwa kukodisha baadhi ya ofisi kwa taasisi zilizomo wilayani humo.
“Pamajo na kuhakikisha mnatoa huduma bora kwa wananch lakini pia mnapaswa kuhakikisha mnapima viwanja vyo vinavyozunguka eneo hili ili kuepuka ujenzi holela” Alimalisisitiza Mhe.Mkuu wa Mkoa.
Akiwa katika Hospitali ya Wilaya Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara alimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuanza kuleta watumishi ili huduma nyingi zianze kutolewa Hospitalini hapo huku wakisubiria TANESCO ilete umeme.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa yupo katika ziara ya kukagua miradi ya maji inayotekelezwa na Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) katika wilaya zote za Mkoa wa Manyara.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.