Agosti 7, 2024 Katibu Tawala Mkoa wa Manyara Bi. Maryam Muhaji ameongoza kikao ambacho kimehudhuriwa na wakurugenzi, Maafisa Elimu Sekondari, Waratibu wa miradi ya SEQUIP, Maafisa Manunuzi, Wahandisi, Maafisa TEHAMA na Wakuuu wa Shule zenye miradi hiyo. Katika kikao hicho mikakati ya utekelezaji wa miradi ya SEQUIP imejadiliwa ambapo miradi iliyopokea fedha katika mwaka wa fedha 2023/2024 na inapaswa itatekelezwa ni;
Ujenzi wa shule ya wavulana ya mkoa itakayo jengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati. Mradi huu umepokea jumla ya fedha kiasi cha Tsh 4,100,000,000
Ujenzi wa shule ya Amali Katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu. Mradi huu umepokea jumla ya fedha kiasi cha Tsh 1,600,000,000
Ujenzi wa Shule ya wasichana ya Mkoa awamu ya pili. Shule imejengwa katika Halmasahuri ya Babati mji na imepokea kiasi cha Tsh 1,100,000,000
Ujenzi wa shule mpya saba za kata, kila moja imepokea Tsh 584,280,029 jumla ni Tsh 4,089,960,203 kwa shule zote saba katika Mkoa wa Manyara.
Ujenzi wa Nyumba za Walimu two in one kwa kila Halmashauri kila nyumba imepokea Tsh 98.000.000 jumla zimepokelewa Tsh 686,000,000
Ujenzi wa mabweni, madarasa na matundu ya vyoo katika Halmashuri za Babati Mji, kiteto, Mbulu Mji, Simanjiro, babati Wilaya na Hananang na kiasi kilicho pokelewa ni Tsh 3,492,300,000
Kwa ujumla fedha iliyopokelewa kwa Miradi hii yote ni kiasi cha fedha Tsh 15,068,260,230 kwa Mkoa wa Manyara.
Aidha, Bi. Muhaji amewasisitiza Wakurugenzi na watendaji wengine katika Halmashsuri kuhakisha wanasimamia kikamilifu na kwa uadilifu matumizi ya fedha hizi ili kufikia malengo ya Serikali yaliyokusudiwa. “Hakikisheni mnasimamia kikamilifu na kwa uadilifu matumizi ya fedha hizi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na Serikali, na mimi mwenyewe nitakikisha nimefika katika maeneo ya Miradi kujionea utekelezaji. Nasisitiza nilazima kuweka mikakati ya kukamilisha miradi ambayo haikukamilika kwa mwaka wa fedha uliopita kabla ya Novemba 2024, ili miradi hiyo ianze kutoa huduma kama ilivyo kusudiwa”. Alisema.
Mtakumbuka kuwa mnamo tarehe 22 July 2024 katika kikao kazi kwa njia ya mtandao Mh. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa Kasimu (Mb) alitoa maelekezo kwa Wakuu wa Taasisi kuhakikisha kuwa Miradi yote iliyopokea fedha kuanzia mwaka wa fedha 2021 hadi sasa ikamilike kabla ya Desemba, 2024. Kwa kuzingatia maelekezo hayo Mkoa umeweka malengo ya kuhakikisha miradi hii inakamilika kabla ya Novemba ,2024.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.