• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

Sikuya wauguzi Duniani 2020,kufanyika mkoani Manyara kitaifa

Imechapishwa Tarehe: January 17th, 2020

Maadhimisho ya siku ya Wauguzi na wakunga duniani yanayofanyika kila inapofika Mei 12, mwaka 2020 kitaifa yamepangwa kufanyika mjini Babati katika mkoa wa Manyara ambapo mgeni rasmi atakuwa kiongozi mkubwa wa Kitaifa.

Akizungumza na wadau mbalimbali mkoani Manyara,Makamu wa rais wa chama cha wauguzi Tanzania Ibrahim Mgoo, amesema maazimisho haya yataenda sambamba na Jubilei ya miaka 200  tangu kuzaliwa kwa mwasisi wa taaluma hiyo Bi. Florence Ningt Ngale aliezaliwa 12-5-1820 huko nchini Italia .

Amesema katika sherehe hizo,kutahitimishwa kampeni ambayo imekuwa ikiendeshwa tangu January mwaka jana  yenye jina 'Nursing Now Campaign" ambayo ilikuwa inalenga kuinua hadhi ya Uuguzi duniani,kuonyesha jamii na taasisi zake zote thamani ya kuwepo kwa Taaluma hiyo Muhimu Ulimwenguni.

Katibu Mwenezi msaidizi  wa chama cha wauguzi TANNA Bi.Johari Yusuph, amesema hiyo itakuwa ni nafasi kwa watakaohudhuria kwani mkoa huo una vivutio vingi na ni rahisi kufikika kwa urahisi katika mikoa yote kutokana na Miundo bora ya barabara.

Naye Mganga mkuu wa wa mkoa wa Manyara Dr. Damas Kayera akizungumza na wadau mbalimbali wa Maendeleo mkoani Manyara, amewakaribisha wakunga wote hapa nchini na kuwahakikishia kuwa Mkoa umefanya maandalizi ya  kutosha ili maadhimisho hayo yaweze kufana.

Zaidi ya shilingi milioni 89 zinahitajika ili kuweza kufanikisha hilo, huku watu zaidi 1000 kutoka maeneo mbalimbali ya nchi na nje ya mipaka wakitarajiwa kuhudhuria siku hiyo Muhimu duniani.

Ni mara ya kwanza Kufanyika kwa maadhimisho haya mkoani Manyara,mwaka jana yalifanyika katika mkoa wa Katavi.

Wakazi wa mkoa wa Manyara wanaojishughulisha na utoaji huduma ya vyakula,Usafiri, huduma za kifedha na kulala wageni watanufaika na Maadhimisho hayo kiuchumi.

Aidha huduma mbalimbali za vipimo zitatolewa bure kwa wananchi wote watakaohudhuria siku hiyo.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.