MKUU wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti amesema hana nia wala lengo la kumdondosha mtu kwenye nafasi yake kwa sababu hiyo sio kazi yake.
Kauli hiyo ameitoa katika kikao cha baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Babati cha kujadili na kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambapo amesema yeye hashughuliki na mtu.
“Sina nia wa lengo la kumdondosha mtu kwenye nafasi yake kwa sababu hiyo sio kazi yangu kama mtu anaona dalili za kushindwa asitafute sababu ya kinga kwamba Mnyeti ndiye anayenishughulikia mimi sishughuliki na mtu mimi nina shughulika na maendeleo ya watu wa Manyara.
“Labda ukanyage waya wakati nahangaika na maendeleo halafu wewe unakanyaga waya ule ninaohangaika nao hapo maana yake tutalipuana lazima shoti itokee.
“Mimi nikiwa nahangaika na shida za wana Manyara wewe kaa pembeni, nikikushirikisha sawa nisipokushirikisha niache niendelee, ninapohangaika na shida za watu wa Manyara halafu wewe unakuja mbele kuziba lazima nitakufyatua,” Amesema Mnyeti.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Babati Nicodemus Tarmo amesema muda uliopo ni wa kuchapa kazi na amemuomba Mkuu wa mkoa aendelee kuwasaidia na wao watamsaidia kuona kazi yake inafanikiwa.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.