Mkuu wa jeshi la polisi Mkoa wa Manyara ACP George Katabazi amefanya mkutano na waandishi wa habari tarehe 14/7/203 saa tano asubuhi, Akitoa taarifa kwa wanahabari kuhusu maendeleo ya shughuli zinazofanywa na jeshi hilo katika Mkoa wa Manyara.
Amewaambia waandishi wa habari tarehe 13 julai majira ya saa tano asubuhi jeshi la polisi Mkoa wa Manyara limefanikiwa kukatamata wahamiaji haramu 12 raia wa Ethiopia ambao ni 1. Kliu s/o Teketl, 2. Chrente s/o Alamu, 3. Tadele s/o Alem, 4. Yofesu s/o Ayano, 5. Workine s/o Balechui, 6. Adana s/o Aranga, 7. Yones s/o Lama, 8. Baraka s/o Gadafa, 9. Samweli s/o Yemeke, 10. Algeze s/o Arenga, 11. Maratu s/o Watso , 12. Buruk s/o Charine.
Wote nikutoka nchini Ethiopia watuhumia walikuwa wakisafirishwa kwa gari aina ya MARK X yenye nambari T. 215 DDY, iliyokuwa ikitokea Mkoa wa Arusha kwakupitia barabara kuu ya Arusha –Babati, Polisi waliweka mtego wakuikamata gari hiyo hata hivyo dereva wa gari hilo alipogundua anafuatiliwa alichepuka kutoka barabara kuu nakuingia barabara ya changarawe inayoelekea kijiji cha chemchem ambako ndiko wahamiaji hao walipokamatwa.
Pia muda wa saa 19:45 maeneo ya kijiji cha kiongozi barabara kuu ya Babati Arusha kata ya Maisaka wilaya ya Babati, Jeshi la Polisi walifanikiwa kukamata dawa za kulevya aina ya Mirungi kiasi cha bunda 264 sawa na kilogram 110 zikiwa zimehifadhiwa ndani ya magunia manne ya katani.
Dawa hizo zilikuwa zikifasirishwa kwa gari aina ya Toyota Noah yenye nambari za usajiri T. 465 CUS iliyokuwa inatokea Mkoa wa Arusha kwenda Babati jeshi la polisi walipata taarifa na kuweka mtego kwa gari hilo.
Dereva mala baada yakugundua gari hilo linafuatiliwa aliongeza kasi na badae alishuka nakukimbia pasipo julikana, juhudi za kumtafuta dereva huyo wa gari Aina ya Noah zinaendelea kufanywa na jeshi lapolisi Mkoa wa Manyara.
Aidha ACP George katabazi amewataka wananchi wa Mkoa wa Manyara kutoa ushirikiano katika kutoa taarifa za wahalifu hususani usafirishaji wa dawa za kulevya, Na wahamiaji haramu ili jeshi la polisi Mkoa wa Manyara liweze kuwakamata nakuwashughulikia kisheria.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.