Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga leo Julai 25, 2024 amezindu Mradi wa USAID wa Rural Evidence and Learning for Water (REAL-Water) kupitia Mfuko wa Udhamini wa Ubora wa Maji nchini Tanzania, mpango huu unaolenga kusaidia vipaumbele vya Sekta ya Maji vya kutoa huduma za maji vijijini na kuhakikisha usalama wa maji kwa kuboresha mbinu za kupima na kutibu maji ili yakifika kwa walaji yawe safi na salama.
Akiwa katika ufunguzi huo RC Sendiga ameihakikushia Real Water kuwa Mkoa wa Manyara kupitia RUWASA utatekeleza mradi huo kwa ufanisi mkubwa na kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa ili mradi huu uweze kunufaisha Wananchi wa Mkoa wa Manyara.
Aidha, RC Sendiga ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwavutia wafadhili pamoja na kutenga fedha kwa ajili ya uboreshaji na usambazaji wa huduma za maji kwa ajili ya matumizi ua binadamu na mifugo. Ameeleza yote hayo yanafanyika kwa shabaha ya kumtua mama ndoo kichwani.
Sambamba na hilo ameipongeza USAID kwa kuwa miongoni mwa washirika wakubwa wa maendeleo wanaosaidia jamii ya Watanzania kwa kufadhili miradi ya Sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya na Maji.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa huduma za sheria Wizara ya maji Ndg. Saimon Nkanyemka amesema Wizara itaendelea kutoa ushirikiano kwa wadau wote watakaojitokeza kushirikiana na Wizara ya maji kwenye utoaji na usambazaji
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.