Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC) jana tarehe 13 Machi, 2020 ilifanya ziara katika Mkoa wa Manyara kwa kutembelea miradi ya maendeleo iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati na Halmashauri ya Mji wa Babati.
Wakiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati wabunge hao walitembelea Kituo cha Afya cha Nkaiti kilichopanuliwa kutoka zahati na kuwa kituo cha Afya. Wabunge hao walipongeza sana Serikali kwa kujenga kituo hicho karibu na jamii za wafugaji kwani kitaondoa usumbufu kwa wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma.
Kituo hicho cha Afya Nkaiti kimetumia jumla ya shilingi Milioni mia nne kwa kujenga jingo la Maabara, jingo la Mama na Mtoto, Nyumba ya kuhifadhia maiti na Nyumba ya Mtumishi.
Akiongea kuhusu changamoto za umeme katika kituo hicho Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Manyara amesema umeme unarajiwa kifika kituoni hapo ndani ya wiki mbili ili kuhakikisha huduma zote zinapatikana.
Mjumbe wa Kamati Mheshimiwa Chrispher Chiiza alishauri pamoja na uvunaji wa maji ya Mvua kituoni hapo lakini ipo haja ya Halmashauri kuhakikisha inachimba kisima ili kuwa na uhakika wa upatikanaji wa maji muda wote kwani maji ya mvua hayawezi kukidhi matumizi kwa mwaka mzima.
“Nawashauri Mchimbe kisima katika eneo hili ili kuwe na maji ya uhakika badala ya kutegemea maji ya Mvua kwani maji ya mvua hayawezi kukidhi mahitaji ya wagonjwa kwa mwaka mzima” Alisema Mheshimiwa Chiiza.
Kwa upande wa Mheshimiwa Mollel ambeye pia ni Mjumbe wa Kamati hiyo alishauri ifanyike tathmini ya maji kati eneo hilo kwani eneo hilo lina asili ya maji chumvi.
Pia Wabunge hao walishauri njia za kutembelea kwenda kwenye Nyumba ya Kuhifadhia maiti ijengwe ili kuepuka ufumbufu.
Katika mradi wa maji wa Minjinga- Darakuta wabunge hao walishauri kazi zinazoanzwa na wakandarasi zimalizwe ili kuepuka matumizi mabaya ya fedha za Serikali na gharama kubwa za mradi kwa kutumia wakandarasi zaidi ya mmoja.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.