Balozi wa Indonesia nchini Tanzania amewaahidi wafanyabiashara Mkoani manyara kuwaunganisha na wafanyabiashara wa nchi ya Indonesia ili waweze kufanya biashara kwa pamoja na kuendelea kujenga mahusiano kati ya nchi ya Tanzania na Indonesia.
Akizungumza katika mkutano na wafanyabiashara wa mkoani Manyara jana katika ziara yake ya kuangalia fursa za biashara na uwekezaji yenye nia ya kuboresha uhusiano wa nchi hizo kiuchumi alisema wafanyabiashara wanafursa nzuri ya kufanya biashara na nchi ya Indonesia kwani nchi hiyo ni miongoni mwa nchi zilizoendelea huku zikiwa na fursa nyingi ikiwa na kutengeneza mashine mbalimbali za uchakata nafaka na zana za kilimo.
Balozi huyo alisema kwa sasa biashara inayofanywa kutoka Indonesia kuja Tanzania haifiki kwa walengwa moja kwa moja na badala yake kumekuwa na walanguzi ambao wanaziongeza gharama na kuziuza bidhaa hizo kwa wafanyabiashara jambo ambalo kwa sasa anataka kuliondoa kwa kuwaunganisha wafanyabiashara moja kwa moja kutoka Indonesia.
“Kwa Sasa ni Bidhaa hamsini tu za Indonesia zianazoletwa Tanzania ambazo ni mafuta ya mawese, Makaratasi, Tanzania inapeleka Tumbaku, Pamba,Karafuu na Mwani’’
“Serikali ya sasa inataka kutumia mahusiano ya kisiasa kuwa ya kiuchumi ili kuifanya Tanzania kuwa chi ya viwanda na uchumi wa kati hivyo ziara yangu itasababisha uhusiano mzuri kati ya wanfanyabiashara
wa Manyara na Mkoa mmoja wa Indonesia , ntatembelea mikoa yote 31 kuangalia fursa mbali mbali na huu ni mkoa wangu wa 13” alisema.
Naye Afisa wa Wizara ya Mambo ya nje Rwangisa Francis alisema kuwa kuwa balozi huyo amefika mkoani hapo kwaajili yabuwekezaji wa viwanda na biashara na hatua hiyo iimekuja mara baada ya balozi huyo alipokuwa
akiwasiliosha hati zake za utambulisho mwaka 2017 kwa Rais wa Jamhuri ya muunganno wa Tanzania Dkt John P. Magufuli na kumuahudi kuwa kwa kuwa Tanzania ni nchi ya viwanda na wao Indonesia wataisaidia kuwa nchi ya viwanda.
“Mikoa ya Tanzania 31 na Indonesia kuna mikoa 34 sasa anapokuja katika mkoa flani anaangalia fursa mbali mbali za zinazojitokeza za uwekezaji na biashara akishaziona anakwenda kule kwao anazungumza na wahusika na kuangalia mikoa inayolingana kifursa na kuiunganisha ili waweze kufanya biashara na kuzalisha’’ alisema Francis.
Alisema kufuatia ziara hiyo anatarajia kama zoezi hilo litafanikiwa atawaleta wawekezaji watakaowekeza kwa makubaliano au wawekezaji wa moja kwa moja ili watanzania waweze kufanya biashara , ikiwa ni pamoja na kuongezeka idadi ya viwanda na ajira.
Kwa upande wake katibu wa Chama cha Wafanyabiashara Mkoani humo TCCIA Mwanahamisi Husen alisema ujio wa balozi huyo mkoani hapo umeleta matumaini kwani balozi huyo ameahidi kuunganisha TCCIA ya Mkoani manyara na ya mkoa mmoja wa Indonesia ili waweze kufanya kazi kwa pamoja na kuwatafutia wafanyabiashara fursa mbali mbali.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.