Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mh.William Ole-Nasha ametoa maagizo kwa Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mh.Chelestine Mofuga kuwachukulia hatua watumishi watano wa serikali akiwemo msimamizi mkuu wa mradi wa ujenzi ambaye ni fundi sanifu Moses Nguvava, Mkuu wa shule ya sekondari Tumati Bw.Killian John, Afisa Elimu sekondari Bw.Ludovick longino ,Afisa ugavi wa Wilaya Bw Faustine Safari na Mwenyekiti wa bodi ya shule ambaye ni mwakilishi wa wananchi Byrson Panga.
akitoa taarifa ya ujenzi kwa fundi sanifu ambaye ni msimazi mkuu wa mradi huo alisema fedha zilizoletwa na Wizara zilikuwa kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 3, bweni 1 na matundu ya vyoo sita ila wao kwasababu walikuta baadhi ya majengo yamekwisha jengwa na wananchi hivyo waliamua kufanya ukarabati na kukamilisha bweni moja na kuweka samani, madarasa manne ambayo yamegharimu jumla ya shilingi milioni 29 kuongeza vyoo na mabafu kwenye mabweni million 18 na kukamilisha maktaba ambayo imegharimu million 15.
Awali kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Mkuu wa wilaya ya Mbulu Mh.Mofuga alisema “Serikali imetoa hizi hela kwa kusaidia na kuongeza nguvu kwa wananchi nimesikitishwa na matumizi haya hivyo nakuagiza OCD kuwakamata wahusika wote wa ujenzi ndani ya masaa arobaini na nane na baada ya hapo wafunguliwe mashtaka kwa mujibu wa sheria na pia nawaagiza TAKUKURU kufanya uchunguzi wa kina namtaka Mkurugenzi aniletee taarifa ya kina juu ya mradi huu”alisistiza
Aidha akizungumza na watumishi wa shule,wanafunzi,wananchi pamoja na viongozi wa serikali alipokuwa akikagua mradi wa ujenzi katika shule ya sekondari Tumati Mh .Naibu Waziri alisema “ huu ni utumiaji vibaya wa fedha za serikali kwani jumla ya million 141 zilitolewa kwa ajili ya ajili ya ujenzi wa madarasa 3 mapya , bweni1, na matundu sita ya choo haziwezi kutumika kukarabati majengo ambayo tayari yamejengwa kwa nguvu za wananchi hivyo nimesikitishwa sana na matumizi haya ya fedha kwani wametumia nyingi hivyo serikali ya awamu ya tano haiwezi kuvumilia ubadhilifu wa fedha na hatua zitachukuliwa iwe funzo kwa wengine.
Akihitimisha ziara yake katika Halamashauri ya Wilaya ya Mbulu aliwataka wanafunzi kusoma kwa bidii na kuzitumia rasilimali zinazoletwa na Seikali kwa ajili ya manufaa yao, pia alizitaka Halmashauri zote kuzitumia vizuri fedha wanazopewa na serikali pamoja na kufuata maagizo ya wizara na vilevile aliwataka wananchi wa eneo hilo kuendelea kuwapeleka watoto shule kwani wakiwaacha nyumbani wanawanyima haki yao ya msingi ya kusoma.
(Kwa Picha mbalimbali angalia Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha)
Imeandikwa na Isabela Joseph (UDSM-Mafunzo kwa Vitendo)
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.