• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Kilimo
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Fomu za Kujiunga na Bangdalalu Sekondari
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Habari
  • Blog

Watumishi waaswa Kuzingatia Sera ya Ugatuaji katika kazi zao

Imechapishwa Tarehe: January 11th, 2019

Watumishi wametakiwa kuwa na uelewa wa kazi wanazofanya kuanzia ngazi ya kijiji hadi Taifa ili kuimarisha uratibu mzuri, uwazi, utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku na kufanya watanzania wajivunie uwepo wao katika nafasi hizo.

Hayo yamebainishwa jana tarehe 10 mwezi wa kwanza 2019  na Naibu Katibu Mkuu (Afya) Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dkt.Dorothy Gwajima wakati wa kikao chake cha kwanza baada ya mapokezi yaliyohudhuriwa na menejimenti na watumishi wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI jijini Dodoma leo.

“Sisi watumishi ndio ramani ya watanzania kuweza kufikia chachu ya maendeleo ya nchii hii, hivyo tukiratibu na kutekeleza majukumu yetu kwa ufasaha ni haki yetu kupata matokeo chanya ya maendeleo ya nchi hii” Amesema Dkt.Gwajima.

Dkt.Gwajima amesema lazima serikali ijenge mfumo mzuri wa uratibu na utekelezaji wa majukumu yake kuanzia ngazi ya kijiji hadi Taifa kwani ndio njia stahiki ya kuweza kupata Tanzania yenye maendeleo na kufanya watanzania kujifunia Utanzania wao.

Akiongea katika kikao cha menejimenti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI wakati wa kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu (Afya) Dorothy Gwajima, Kaimu Katibu Mkuu Tixson Nzunda Ofisi ya Rais - TAMISEMI), amesema ili mtumishi wa Umma aweze kutimiza majukumu yake ya kila siku ni lazima atambue kuwa yeye ni wakili wa anaowahudumia, mratibu wa matokeo chanya, awe mcheshi kwa jamii anayoihudumia na yeye ajihisi ni sehemu moja wapo ya jamii hiyo.

Katika hatua nyingine kwenye kikao maalum na watumishi wa Idara ya Afya, Dkt. Gwajima amewaasa watumishi wa Idara ya Afya Ofisi ya Rais -TAMISEMI kuuvaa uhusika wa jamii wanayoitumikia katika kutekeleza majukumu yao ili kupata chachu ya kufanya kazi kwa ufanisi, juhudi na kutoa huduma bora kwa watanzania.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Dkt. Ntuli Kapologwe amempongeza Dkt. Gwajima kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo kwa niaba ya Idara yake ambapo ameahidi watampa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora za afya kuanzia ngazi ya kijiji hadi Taifa na kwamba wapo tayari kupokea maelekezo yote ya Serikali.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wakurugenzi na watumishi wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mkurugenzi wa Kitengo cha Ukaguzi na Ufuatiliaji wa Fedha katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa OR-TAMISEMI Miriam Mmbaga amesema kuwa ameguswa na mfumo aliokuja nao Dkt. Gwajima wa kutaka uratibu, uwazi, utekelezaji na ugatuzi wa madaraka kuanzia ngazi ya kijiji mpaka Taifa na kwamba utaleta chachu ya matokeo bora katika kutekeleza majukumu yao.

Dkt.Gwajima ameteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapo jana kuwa Naibu Katibu Mkuu (Afya) Ofisi ya Rais TAMISEMI ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi wa Tiba wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Imeandikwa Na: Majid Abdulkarim na Fred Kibano (OR-TAMISEMI)

Matangazo

  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2021 MKOA WA MANYARA December 18, 2020
  • MAJINA YA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI JIMBO LA BABATI MJINI October 21, 2020
  • MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2018 MKOA WA MANYARA December 27, 2017
  • OR-TAMISEMI YATANGAZA AJIRA MPYA ZA WALIMU WA MSINGI NA SEKONDARI JULAI 2018 July 17, 2018
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • RC Manyara amaliza Mgogoro wa ardhi baina ya mwekezaji na wananchi

    September 01, 2021
  • Mkirikiti amkabidhi Makongoro Ofisi rasmi

    May 25, 2021
  • Karibu Manyara Mhe. Makongoro Nyerere!!!

    May 22, 2021
  • Tuweke uzalendo ktk kusajili watoto chini ya miaka mitano - RC Manyara

    April 20, 2021
  • Tazama Zote

Video

Asilimia mbili ya mikopo kwa walemavu
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

    Barabara ya Babati - Singida

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 310

    Simu ya mezani: 027-2510066

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: rasmanyara.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2021 Manyara Region . All rights reserved.