Mkuu wa wilaya ya Babati Mheshimiwa Elizabeth Kitundu amewataka wazazi na walezi kuhakikisha watoto wote waliofaulu darasa la saba wanaendelea na elimu ya Sekondari huku kidato cha nne ambao hawatafanikiwa kuendelea kidato cha tano wakiendelea kupata mafunzo katika vyuo vya Ufundi stadi (VETA).
Mkuu wilaya ametoa wito huo alipokuwa akizungumza na wanafunzi,walimu na wazazi katika mahafali ya 10 kwa shule ya Msingi Rift Valley Babati na ya 5 kwa upande wa Sekondari Rift Valley Babati ambapo amesema baada ya matokeo mwanafunzi akiwa hajapata alama za kumwezesha kuendelea na kidato cha tano asikate tamaa kwani kuna vyuo vya ufundi stadi ambavyo vinatoa mafunzo mbalimbali yatakayowasaidia katika maisha yao.
Mkuu wa wilaya akawatia moyo walimu kuongeza bidii katika kufundisha na kuzingatia maadili mema huku akiwasihi wanafunzi kusoma kwa bidii ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao.
Mkurugenzi wa taasisi za Rift Valley shule ya msingi The Moshi Academy, Northern Highlands Secondary School (NHSS),North Highlands Teachers Training College Henry Stansalaus Mallya,amesema katika taasisi zake walimu watakaobainika wanakwenda kinyume na maadili wanachukuliwa hatua mbalimbali ikiwemo kuachishwa kazi.
Mkuu wa shule ya Rift Valley Babati Sekondari Daddly Wilfredy amesema shule hiyo ilianza mwaka 2003 na kupokelewa rasmi na mmiliki wa sasa mwaka 2012 baada ya waanzilishi kushindwa kuiendesha huku ikiwa na mafanikio makubwa katika taaluma kwa kufaulisha wanafunzi katika madaraja ya juu ambapo wengi wao wamekuwa wakichaguliwa kujiunga katika shule za Sekondari.
Mwalimu mkuu Dadly amesema mahafali hayo ni ya tano kwa Sekondari huku kukiwa na mafanikio makubwa,ambapo kwa jitihada za walimu wazoefu walionao,shule imekuwa ikifanya vizuri Kimkoa na Kiwilaya nfasi ya tatu nay a nne kila mwaka.
“Kwa kweli tuna kamati ya kuchuja sana watumishi,akitokea mmoja kwa bahati mbaya akafanya tabia zisizofaa hata kama hatuna uthibitisho,tunamchukulia hatua za papo kwa papo”.alisema Mallya.
Imeandikwa Na: John Walter
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.