• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

Waziri Mhagama azindua wiki ya vijana kitaifa na kitabu cha mwongozo wa uwekezaji Mkoani Manyara

Imechapishwa Tarehe: October 10th, 2023

Na Nyeneu, P. R - Mjini Babati

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama amezindua kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Manyara sambamba na Wiki ya Vijana katika Wilaya ya Babati Mkoani Manyara.Muongozo huo unaelezea kwa kina fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo Mkoani Manyara na Dira ya Mkoa kwenye eneo la Uwekezaji na Maendeleo.Uzinduzi huo uliofanyika katika Wiki ya Vijana Kitaifa 2023 iliyoanza Oktoba 8, 2023 inatarajiwa kumalizika Oktoka 14, 2023 ambapo itaenda Sambamba na Uzimaji wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa katika mkoa huo.

Akizungumza katika Uzinduzi huo Waziri Mhagama ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu Mhe. Khasim Majaliwa amefurahishwa na mwamko wa Vijana jinsi walivyojitokeza kuhudhuria katika Wiki yao inayowapa fursa ya kutambua mambo mbali mbali yanayofanywa na vijana wenzao Tanzania nzima.

"Binafsi nimefurahishwa na muamko wa vijana jinsi mlivyojiyokeza na kuonyesha kazi zenu, nimepita katika mabanda mbali mbali nimejionea kazi zenu za mikono na kwakweli vijana ni nguvu kazi ya Taifa letu," amesema Waziri Mhagama.

Waziri Mhagama alitoa pongezi kwa Viongozi wa Mkoa wa Manyara unaoongozwa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Queen Cuthbert Sendiga kwa jinsi walivyojipanga kusimamia na kufanya maandalizi ya shughuli mbalimbali za kiserikali ikiwemo Wiki ya Vijana, Ibada ya Kitaifa ya kumbukizi ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga amesema kuwa mkoa wa Manyara unamaono makubwa sana katika kupambanua fursa zilizopo hivyo ni vyema vijana wakawa msitari wa mbele katika kuchangamkia fursa hizo.

"Nawashukuru timu nzima ya Mkoa wa Manyara kwa kazi nzuri na kubwa tulioshirikiana kwenye uzinduzi wa jarida hili, tunaweka mazingira rafiki kwa kila atakayetaka kuwekeza ndani ya Mkoa wetu wa Manyara na tumeanza kutangaza fursa hizi kwa vijana wetu waliofurika mjini Babati kutoka pande zote za Tanzania," amesema Mhe. Queen.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama ,Taasisi, na Dini. Wiki ya Vijana Kitaifa 2023 inaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu yakiwa na Kauli mbiu, "Vijana na Ujuzi Rafiki wa Mazingira kwa Maendeleo Endelevu"

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.