• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

Waziri Mkuu ashusha Neema kwa Maafisa Ustawi wa Jamii

Imechapishwa Tarehe: January 31st, 2019

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameziagiza Wizara ya Ofisi ya Rais, Tamisemi na ile ya Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto kukutana na kupitia muundo wa utumishi kwa maafisa ustawi wa jami ili kuwawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Ustawi wa Jamii wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika kwa siku tatu kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete uliopo Jijini, Dodoma.

Wizara hizi mbili zikutane na kuangalia namna bora ya kubadili muundo wa maafisa hawa ili kuwatengenezea mazingira mazuri kwa ajili ya kazi yao.

“Maafisa Ustawi ni watu muhimu sana kwenye jamii ni muhimu nafasi yao iwekwe vizuri kwenye muundo na kama italazimu kubadili muundo ili kazi yao ifanyike vizuri mfanye hivyo  na kama ni suala linalohitaji marakebisho ya sheria mlete na bahati nzuri hapa tuna mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe Jason ( Mb) litafanyiwa kazi” alisema Mhe Majaliwa.

Wakati huo huo Waziri Mkuu Majaliwa  amekemea tabia ya halmashauri kuwataka watu wenye ulemavu kutoa asilimia 10 ya mkopo wanaochukua kama dhamana wakati wa kupewa mikopo.

“Kuna mbunge amesema kuna halmashauri zinawataka watu wenye ulemavu kutoa asilimi 10 ya thamani ya mkopo wanaochukua kama depost, jambo hilo haliwezekani.

Mhe. Majaliwa aliongeza: “ Kuwataka waweke depost hilo jambo halipo na hata Sheria yenyewe haisemi hivyo, hivi watu wenye ulemavu watazipata wapi fedha hizo?

“ Ninyi maafisa ustawi wa jamii hakikisheni mnalisimamia hilo, fedha inatakiwa kutolewa kama sheria inavyoruhusu, na hii si kwa mapenzi ya mkurugenzi au baraza la madiwani.

Serikali iliweka sheria ambayo inazitaka kisheria halmashauri zote nchini kutenga asilimia 10 kutoka kwenye mapato ya ndani kwa ajili ya wanawake na vijana na  asilimia 2 zinaelekezwa kwa watu wenye ulemavu, asilimia nne kwa wanawake na asilimia 4 kwa vijana.

Naye Naibu Waziri wa Tamisemi, Mhe. Josephat Kandege alisema Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kuimarisha sekta ya ustawi wa jamii kwa kutekeleza matakwa ya kisheria yenye dhamira ya kuboresha ustawi wa jamii yetu hapa Nchini .

Alisema tumeandaa  Waraka wa utekelezaji wa Sheria ya Wati wenye Ulemavu Na. 9 ya mwaka 2010 lengo ikiwa ni kuhimiza wajibu wa Wakuu wa Mikoa katika kusimamia utekelezaji wa Sheria Na. 9 ya watu wenye ulemavu.

Pia tumepeleka Waraka wa mwaka 2018 kwa Wakuu wa Mikoa kushughulikia mashauri ya watoto  ili kupunguza ama kuzuia ukatili dhidi ya watoto alisema Kandege.

“Kwa nyakati tofauti bajeti ua utekelezaji wa masuala ya Ustawi wa Jamii umekua ukifungamanishwa pamoja na bajeti ya Lishe , kwa bajeti ya mwaka 2019/20 tumefanikiwa kufanya maboresho ya kimfumo ambapo Bajeti za Ustawi wa Jamii umewekewa dirisha maalumu ndani ya mfumo wa Planrep ambalo linajulikana kama “Council Comprehensive Social Welfare Operatiobal Plan”; Jitihada hizi zitasaidia kuongeza ufanisi katika uwajibikaji wa watendaji, kuweka uwazi na kudhibiti matumizi ya fedha za miradi ikiwemo fedha za wadau wa maendeleo” alisema Kandege.

Naye Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile aliwaagiza maafisa ustawi wa jamii nchi nzima kukaguza vituo vya kulelea watoto ili ambavyo havina sifa na vibali halali vifungwe.

“ Kumekuwa na ongezeko la vituo vya kulelewa watoto yatima, bahati nzuri kuna watu ambao ni waaminifu, lalini kuna wengine wasiowaadilifu, Tumepokea malalamiko kuwa baadhi ya watu wanawatumikisha watoto hao kwenye biashara ya ombaomba, biashara ya ngono na vingine kuwa vituo vya kususanyia watoto kwa ajili ya biashara ya utumwa.

“ Hivyo maafisa wote manatakiwa kuvikagua vituo hivi na visivyo na sifa vifungwe na hakikisheni wanawaletea taarifa zao kila robo mwaka, nusu mwaka na za mwaka mzima.”

Pia Dk. Ndungulile alisema serikali iko katika hatua ya kuandika sheria itakayosimamia sekta hiyo sambamba na uanzishwaji wa Baraza litakalosimamia maadili ya maafisa ustawi wa jamii.

Naye Mwakilishi wa Mkazi wa UNICEF, Maniza Zamani pamoja na kuishauri serikali kuweka mazingira rafiki ya ufanyaji kazi kwa maafisa ustawi wa jamii na kuahidi kuwa wadau wa maendeleo nchini Tanzania wataendelea kuisaidia serikali katika kuimarisha sekta hiyo ili kuboresha utoaji wa huduma.

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Ustawi wa Jamii, Ofisi ya Rais Tamisemi, Rasheed Maftah alisema lengo la mkutano huo ni kukumbushana maadili ya kazi Lengo la kukumbushana maandili ya kazi, uwajibikaji na weledi katika kuhudumia wananchi wenye mahitaji.

“ Pia tumekutana ili kuepana mrejesho wa utekelezaji wa shughuli za ustawi wa jambii kwenye mamlaka za serikali za mitaa na kuwezesha kufahamu mafanikio na

“ Pia kujadili maendeleo na changamoto zinazohusu utoaji wa huduma za ustawi wa jamii katika mikoa na mamlaka za serikali za mitaa na kushirikishana mbinu za utatuzi na hatimaye kupeana uelekeo wa pamoja wa utekelezaji wa mwaka huu wa fedha 2019/2020.

Mkutano huu unaofanyika kwa mara ya kwanza toka majukumu ya ustawi wa jamii yagatuliwe  mwaka 2006 unaenda sambamba na Kauli Mbiu “Uadilifu, Weledi na Uwajibikaji katika utoaji wa huduma za Ustawi wa Jamii Ngazi ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa ni Nguzo katika kuelekeza uchumi wa kati wa viwanda”.

Na:TAMISEMI

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.