Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Joseph Mkirikiti (kushoto) akimwelekeza jambo Waziri wa Kilimo Mhe.Profesa Adolf Mkenda (kushoto) alipotembea Mashamba ya ngano huko Basutu, Wilaya Mkoani Manyara 23 Disemba,2020.
Waziri wa Kilimo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Profesa Adolf Mkenda (Mb) amewataka wakulima wa zao la ngano Wilayani ya Hanang Mkoa wa Manyara kuongeza uzalishaji wa zao hilo kwani Serikali imeamua kwa dhati inaliinua zao na ngano na kuhakikisha wanunuzi wa ngano wanapatikana na wananunua kwa bei nzuri itakayowanufaisha wakulima wa zao la ngano.
Mheshimiwa Waziri ameyasema hayo jana Jumatano alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea na kuona hali ya ulimaji wa ngano na changamoto zinazowakabili wakulima wa ngano katika mashamba yaliyopo Wilayani Hanang katika Mkoa wa Manyara.
Akisoma tarifa kwa Mheshimiwa Waziri Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Hanang Bwana Solomon Sshati alisema kuwa Hanang ina mashamba makubwa sab ana kati ya mashamba hayo mashamba matano wamekabidhiwa wawekezaji,shamba moja libinafsishwa kwa wananchi na shamba moja lenye ekari 13000 limebaki kwa Halmashauri ambalo jumla ya ekari 9000 wanakodisha kwa wananchi kama chanzo cha mapato ya Halmashauri.
Akizungumzia changamoto mbalimbali katika mashamba hayo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Basutu Mhe, Rozi Kamili Sukum amemwambia Waziri kuwa wakulima wengi wameamua kulima Alizeti,Mahindi,Maharage kutokana na ngano kuwa na bei ndogo.
“Mheshimiwa Waziri Wakulima wengi wameacha kulima ngano kwa sababu ngano haina bei na kwa sasa kuna mnunuzi mmoja tu kwa hiyo hana mshindani, ananunua kwa bei anayotaka”Alisema Mheshimiwa Rozi.
Akizungumzia changamoto hizo Mhe.Wazir wa Kilimo amewataka wakulima wakubwa na wakulima wadogo wate wa ngano huko Basutu kuhakikisha mashamba yote yanalima ngano na asiyelima ngano wizara itaangalia namna ya kubadilisha ulimiki wa mashamba hayo kwani kwa sasa Wizara imeingia makubalino na wanunuzi wa ngano kununua ngano yote inayolimwa Tanzania na hawatanunua ngano nje ya nchi mpaka wamalize kununua ngano ya nchini.
“Sasa hivi soko la uhakika la ngano lipo kwa hiyo tunahitaji ardhi yote ilimwe ngano,sisi tutaingia makubaliano na wale wote wanaoagiza ngano nje ya nchi kuhakikisha kabla ya kununua ngano ya nje ya nchi ni lazima ngano ya ndani iwe imeisha yote na wameahidi kununua kwa bei nzuri itakayowanufaisha wakulima wetu” Alisema Mhe.Waziri.
“Na tukikuta ardhi haujatumiwa kwenye ngano tutaomba maamuzi ya kutengua umiliki ili tutafute mtu mwingine kwa sababu tunataka mashamba yote yalimwe ngano msimu ukianza” Aliongeza Mheshimiwa Waziri.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe aliwataka wamiliki wa Kampuni ya Ngano Ltd inayomiliki ekari 40000 za mashamba, kuwaachia wananchi kiasi cha ekari ili shamba lote lilimwe kwa kuwa wao hawana uwezo wa kulima eneo lote na hivyo kusababisha eneo kubwa kubaki bila kulimwa.
“Viongozi wa Mkoa wa Manyara kaeni na Wamiliki wa Ngano Ltd,Uongozi wa vyama vya ushirika ili muone namna gani mnaweza kuchukua sehemu ambayo Ngano Ltd hawezi kulilima ili muwakatikie wakulima maeneo ili walime bila kuhamisha umiki kwani serikali inataka kuona mashamba yote ya ngano yanalimwa” Alisema Mhe. Naibu Waziri.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Profesa Siza Tumbo alisema kuwa kwa kuwa ukulima wa zao la ngano ni lazima uwe na maeneo makubwa na unahitaaji mitambo wao watahakikisha wanaleta wataamu kutoka Wizarani na KAMATEC ili kufanya tathmini ya mitambo iliyopo na kuangalia namna ya kuifufua ili wakulima wa ngano wapate uhakika wa kulimiwa na kupandiwa mashamba yao.
Mheshimiwa Waziri wa Kilimo pia alikutana na wakulima wa ngano katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Msingi Katesh A na kuwahakikishia jinsi Serikali ilivyojipanga kufufua zao la ngano katika Mkoa wa Manyara.
Ziara hiyo ya Waziri wa Kilimo, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof.Siza Tumbo na Maafisa wengine kutoka Wizarani Mkoani Manyara imekuja baada ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais katika Wizara hiyo moja kati ya kazi walizopewa ni kuhakikisha wanashughulikia zao la ngano. Mkoa wa Manyara hasa eneo la Basutu Wilayani Hanang ni moja kati Mikoa inayolima ngano kwa wingi hapa nchini Tanzania.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.