Kuelekea Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Katibu Tawala Mkoa wa Manyara Bi. Karolina Mthapula amefanya ukaguzi wa miradi ya Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Kiteto katika ziara hiyo ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama Mkoa na wataalamu mbalimbali kutoka Ofisi ya Mkoa na mratibu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoa na wa Wilaya ya Kiteto pamoja na Mkuu wa Wilaya ya kiteto Bw. Mbaraka Alhaji Batenga.
Katika ziara hiyo Katibu Tawala ametembelea nakufanya ukaguzi eneo la Dosidosi lililopo Kata ya Dosidosi kijiji cha Dosidosi eneo ambalo yatafanyika makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Dodoma. Mratibu wa mbio
za Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Manyara Samwel Pastory ametoa maelekezo kuhusu mpangilio na utaratibu mzima katika eneo hilo.
Aidha Katibu Tawala Mkoa wa Manyara amefanya ukaguzi wa mradi wa shule ya msingi Esukuta iliyopo kata ya Dosidosi kijiji cha Esukuta, Ambayo imekamilisha mradi wa ujenzi wa madarasa mawili na Ofisi, mradi ambao umetekelezwa kwa fedha za ndani ambapo mradi huo ulinza mwezi julai 2023 na utazinduliwa na Mwenge wa Uhuru tarehe 7/10/2023.
Vilevile amefanya ukaguzi wa Daraja la Orkine lililopo Kata ya Orkine kijiji cha Orkine mradi wa ujenzi wa daraj hilo ulianza Septemba 2022 ambapo mradi huo unatarajiwa kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru. Ujenzi wa daraja hilo utasaidia kuboresha huduma ya usafirishaji wa mazao ya wananchi wa kijiji cha Orkine mradi huo umeleta ajira ya muda kwa vijana wa Wilaya ya kiteto, sambamba na hilo Katibu Tawala Mkoa wa Manyara amefanya ukaguzi wa ujenzi wa shule ya msingi Azimio iliyopo Kata ya Matui kijiji cha Matui.
Pia ametembelea nakufanya ukaguzi wa mradi mkubwa wa maji uliyopo katika kijiji cha Karoleni mradi uliazna Januali 2022 na umekamilika 2023. Ujenzi wa mradi huo ulienda sambamba na ujenzi wa mabomba kwaajili ya kusambaza maji ujenzi wa matenki makubwa mawili ya maji. Mradi huo utasaidi kutatuwa kero ya Maji katika Wilaya ya Kiteto, Pia amefanya ukaguzi wa mradi wa mazingira katika shule ya Sekondari Nasa iliyopo Kata ya Matui.
Ametembelea nakufanya ukaguzi wa mradi wa ujenzi Hospitali ya Wilaya ya Kiteto ambapo ujenzi wa mradi huo nipamoja na majengo ya mama na watoto, jengo la upasuaji mradi ulianza mwezi Februali 2022 utakamilika nakuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru Oktoba 7, 2023, Katibu Tawala Mkoa wa Manyara amelidhishwa na miradi hiyo yote.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.